Saturday, March 11, 2023

WMA yataka mizani ya kupima gesi kwa wauzaji

Wakala wa vipimo mkoa wa Kilimanjaro (WMA) imewataka wauzaji wa gesi za kupikia kuhakikisha wanakuwa na mizani za kupima gesi kwani kwa kutokuwa na mizani ni kosa kisheria.

Hayo yamesemwa Machi jana na Maeneja wa Wakala wa vipimo mkoa wa Kilimanjaro Salum Msinde wakati akitoa.semina kwa wauzaji wa gesi za kupikia majumbani iliyofanyika mjini Moshi mkoani humo.

Masinde amesema ni kosa kisheria wauzaji kuuza gesi bila kuwa na mizani, hivyo wanapaswa kuhakikisha wanakuwa na mizani ili kuepuka hatua kali za kisheria kwa wale watakaobainika kutokuwa na mizani hizo.

Amesema semina hiyo imelenga kuwapa elimu wauzaji wa gesi za kupikia majumbani kutokana na kuweko kwa malalamiko mengi kutoka kwa wananchi ya kuuziwa mitungi ya gesi ikiwa pengufu ya ujazo unaotakiwa kisheria.

Amesema bidhaa yeyote inayouzwa pungufu ina madhara makubwa ya kiuchumi, ambapo muuzaji hawezi kupata kiasi cha fedha alichokuwa amekusudia kukipata, kutopata ushindani ulio sawa sambamba na shughuli za kiuchumi kudorora.

Naye Afisa vipimo Mwandamizi mkoa wa Kilimanjaro Meshack Peter Edward, amesema semina hiyo ni muhimu kwa wauzaji hao wa gesi za kupikia majumbani  kwani itawasaidia kufuata Sheria, taratibu na kanuni za wakala wa vipimo.

Kwa upande wake Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia Uwezeshaji, Viwanda na Biashara Halima Faraji Hassan, ametoa wito kwa Wakala wa vipimo mkoa wa Kilimanjaro kuendelea kutoa elimu kwa wauzaji hao wa gesi na sio kuanza kukimbilia kuwapiga faini kabla hawajawaelimisha madhara hayo.

Amesema kumekuwepo na malalamiko.ya wananchi kuhusiana na kuuziwa bidhaa zilizopungufu pale ambapo wananchi wanapofanya manunuzi yao hivyo mafunzo kama hayo ya mara kwa mara yatawasaidia wafanyabiashara hao kuelewa umuhimu wa vipimo na kufanya biadhara zao kwa anjia.iliyo sahihi.

Afisa Biashara mkoa wa Kilimanjaro James Bwanali, amewataka wafanyabiasha hao wa gesi kuhakikisha kwamba elimu waliopatiwq wanaizingatia ili kuepuka usumbufu wa kukqmatwa na kupigw faini.

Nao baadhi ya wafanyabiashara wa gesi  washiriki wa semina hiyo Evalist Swai na Emmanuel Mero wauomba uongozi wa vipimo mkoa wa Kilimanjaro  kutoa elimu ya vipimo mara kwa mara ili kuweza kuwafikia wafanyabiashara wengi zaidi.

Zaidi ya wauzaji wa gesi za kupikia majumbani 50  kutoka wilaya ya Hai, Manispaa ya Moshi na Wilaya ya Moshi Vijijini amepatiwa semini hiyo iliyoandaliwa na Wakala wa vipimo mkoa wa Kilimanjaro.





0 Comments:

Post a Comment