Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo Liberatus Sabas amewataka
wananchi wanaoishi kandokando ya
barabara kutokuwa na tamaa na kujiepusha na ajali ambazo zinaepukika, pamoja na
kuwataka wale wote waliopata majeraha madogo madogo na kutokomea wasisite kwenda hospitali kwa ajili
ya kupatiwa matibabu.
Ajali hiyo
imetokea majira ya asubuhi katika eneo la Msamvu Mkoani Morogoro na hadi sasa
Jeshi la polisi, limekwishakamata lita takribani 206 za mafuta ya petroli
, zilizokuwa zimefichwa katika mabanda pembezoni mwa eneo la ajali ilipotokea.
Sabas ameitaja idadi ya watu waliofariki katika ajali ya gari iliyoanguka nakulipuka
kwa moto Jumamosi Agosti 10, kuwa ni 62 na majeruhi 72.
ITV imesema idadi ya
vifo imefikia 100 jioni hii, huku vyanzo vingine vikidai kuwa idadi hiyo
inaweza kuongezeka.
0 Comments:
Post a Comment