Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Edward Moringe Sokoine enzi za uhai wao. |
Edward Moringe Sokoine
alizaliwa Agosti Mosi, 1938 katika jimbo la Monduli mkoani Arusha.
Alikulia
katika maisha ya ufugaji katika familia ya mzee Moringe. Mnamo mwaka 1948-1958
Edward Sokoine alipata elimu ya msingi na sekondari hapo hapo Monduli na Umbwe.
Mwaka 1961, alijiunga na chama cha ukombozi (TANU) Baada ya kutoka masomoni
nchini Ujerumani kwa masomo ya Utawala. Kabla ya kuwa waziri mkuu Edward
Moringe Sokoine alipata kufanya kazi mbalimbali kama vile mkuu wa wilaya ya
Msai.
Lakini mwaka 1967 alikuwa msaidizi wa waziri wa mawasiliano, kazi na
usafirishaji. Na mpaka mwaka 1970, Moringe Sokoine alikuwa katika Baraza kuu la
Chama Cha Mapinduzi. Na 13/2/1977, 24/2/198O mpaka 1984, alikuwa waziri mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Historia inasema pia Sokoine alikuwa mbunge wa
kwanza wa jimbo la Monduli na mnamo Aprili 12, 1984 alifariki dunia kwa ajali ya gari iliyotokea
mkoani Morogoro, akitokea mkoani Dodoma.
Aliamini sana vijiji vya Ujamaa kama
sehemu muhimu ya maendeleo ya taifa la Tanzania, alipenda usawa kwa kila mtu na
alipenda watu wathaminiane kwa kila hali.
Hakuwa na mzaha kwenye utendaji wake
na mpaka sasa zipo shule zinatumia jina la Sokoine, zipo barabara, mitaa na kumbi
za mikutano zinatumia jina la Sokoine.
0 Comments:
Post a Comment