Friday, August 23, 2019

Alexei Navalny, mkosoaji mkuu wa Putin aachiwa


Mkosoaji wa serikali ya Urusi, Alexei Navalny ameachiwa huru leo baada ya kutumikia kifungo cha siku 30 jela kwa kupanga maandamano ya upinzani, ambayo yamegeuka kuwa vuguvugu ambalo limeitikisa serikali ya Urusi tangu mwezi uliopita. 

Polisi walikuwa nje ya gereza wakati akiachiwa huru lakini hawakuchukua hatua yoyote ya kumkamata tena, kama walivyofanya wakati viongozi wengine wa upinzani walipoachiwa huru hvii karibuni. Lakini Navalny ameendelea kuwataka wafuasi wake kuingia mitaani, kitu kinachoweza kuwafanya polisi wamkamate tena. 

Mara baada ya kutoka jea, kiongozi huyo wa upinzani na mwanarakati wa kupinga rushwa mara moja alilaani kile alichosema kuwa ni vitendo vya kigaidi vilivyofanywa na serikali ya Urusi katika kuyazima maandamano mjini Moscow katika wiki za hivi karibuni.


CHANZO: DW

0 Comments:

Post a Comment