Tuesday, August 27, 2019

MAKTABA YA JAIZMELA: Lyndon B. Johnson ni nani?

Lyndon B. Johnson alichaguliwa kuwa makamu wa Rais wa 37 wa Marekani mwaka 1960 na alikuja kuwa Rais wa 36 taifa hilo mwaka 1963 baada ya kuuawa kwa Rais John Fitzgerald Kennedy. 

Lyndon Johnson alikuwa akifahamika na wananchi wake kama LB . Akiwa kama Rais wa taifa hilo aliidhinisha Sheria ya Haki za Kiraia ya mwaka 1964 na Sheria ya Kupiga Kura ya mwaka 1965. Pia LB alishinikiza kumalizika kwa Vita vya Vietnam na ushiriki wa Marekani katika vita hivyo. Kabla ya kufa kwake kwa Mshtuko wa Moyo Januari 22, 1973 siku moja kabla LB alikaririwa akisema anaona amani inapatikana Vietnam. Alifariki akiwa na miaka 64. Lyndon alizaliwa Stonewall, Texas Agosti 27, 1908 kutoka kwa wazazi Samuel Ealy Johnson Jr na Rebekah Baines akiwa mtoto wa kwanza kati ya watano ambao walifanikiwa kuwa nao. Familia yao ilikuwa ikijulikana kwa kilimo na ufugaji  jimboni Texas. Baba yake alikuwa miongoni mwa wajumbe wa Congress huko Texas akionyesha siasa safi  kuliko hata  ufugaji licha ya kwamba alishawahi kupoteza shamba la familia wakati Lyndon alipokuwa bado mdogo. Aliingia kwenye siasa baada ya Richard M. Kleberg kushinda uchaguzi mwaka 1931 kuiwakilisha Texas katika Bunge la Wawakilishi. Hivyo Kleberg Jr. aliamua kumteua LB kuwa katibu wake. LB alipata nafasi hiyo baada ya ombi la baba yake na Seneta Welly Hopkins kwani alikuwa akimpigia kampeni mwaka 1930. Mnamo mwaka 1948 Lyndon alishinda uchaguzi wa Bunge la Seneti na mwaka 1951 alichaguliwa kushika wadhifa kuwa msemaji wa bunge hilo kwa watu. Alizidi kupaa katika siasa kutokana na kujituma na hoja zenye msingi kwa tiketi ya chama cha Demokrati. Mnamo mwaka 1960 aliwania uchaguzi wa urais ambao hakufanikiwa kupita. Licha ya kushindwa kupata nafasi ya kuchaguliwa John F. Kennedy alimwita awe makamu wake wakati wa kampeni. Wakati huo JKF alikuwa seneta wa Massachussets. Hivyo wawili hao wakafanikiwa kuwashinda wa upande wa Republican Richard Nixon na mwenzake Henry Cabot Lodge Jr. Novemba 22, 1963 JFK aliuawa na LB akashika wadhifa huo kama Rais. LB aliapishwa ndani ya ndege Air Force One baada ya kuuawa kwa JFK. Mwaka uliofuata LB alifanikiwa kumwangusha seneta wa Arizona Barry Goldwater. Lyndon Johnson aliibuka mshindi kwa asilimia 61.1, kiwango amcho kinachukuliwa kuwa ni cha juu tangu uchaguzi wa mwaka 1820 ambao ulimweka madarakani James Monroe aliyeibuka mshindi kwa asilimia 80.6 dhidi ya chama cha Federalist. 

Johnson anakumbukwa kwa mafanikio yake yote ya kisheria na kutawala kwa makundi. Mnamo 1980, alipewa tuzo ya heshima ya Jimmy Carter na Medali ya Rais ya Uhuru.

0 Comments:

Post a Comment