Thursday, August 15, 2019

Same yapokea msaada wa vitabu vya Sayansi kutoka Uingereza


Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro imepokea shehena ya vitabu vya masomo ya Hisabati, Baiolojia, Chemistry na Fizikia vilivyotolewa na wadau kutoka nchini Uingereza kwa ajili ya wanafunzi wanaosoma masomo ya Sayansi. 

Akizungumza katika hafla ya kupokea msaada huo iliyoenda sanjari na uzinduzi wa Maktaba maalumu ya Sayansi iliyopo katika kijiji cha Goma kata ya Mshewa, Mkuu wa Wilaya ya Same Senyamule amewashukuru wadau wa Word Expedition Exchange kutoka nchini Uingereza kwa msada walioutoa kwani uwepo wa vitabu hivyo, vitahamasisha masomo ya Sayansi kwa wanafunzi wa shule za sekondari za maeneo ya vijijini.

DC Senyamule aliwaomba wadau hao kuendelea kuifadhili wilaya ya Same katika nyanja mbalimbali ikiwemo sekta ya maji na  afya huku pia akitoa wito kwa walimu wa shule za sekondari zilizopo kwenye ukanda huo kuhakikisha kuwa vitabu hivyo vinatumika kuleta matokeo chanya.

“Uwepo wa vitabu hivi utasaidia kupata wataalamu watakaotusaidia kuleta maendeleo katika misingi ya kuwajengea uwezo wa elimu, kwani  tutakuwa na uhakika wa madaktari , mainjinia, tutakuwa na mafundi katika sekta ya kilimo, mifugo na maji hivyo changamoto za wataalamu kwenye maeneo yetu haya tutakuwa tumezitatua ,”alisema DC Senyamule.

Aliongeza kuwa “Nawaomba wanafunzi muwape muda waje wasome vitabu hivi, mimi nilituma wataalamu wangu waje kuviangalia kama vinafaa kwenye mitaala yetu, walinipatia majibu kwamba vitabu  hivyo vinavyofaa,”alisema DC Senyamule.

Alifaanua kwamba kama wataalamu walinithibitishia kwamba ni vitabu vinavyofaa ni wazi kuwa tunawezo wa kuvitunza vitabu hivyo ili vitumike hata wenzetu waliotusaidia kuleta vitabu hivi waweze kuona kuwa kazi yao imekuwa na faida kwa watoto wetu kufaulu vizuri.
Kwa upande wake Mwalimu Gisela Trimo, alisema kuwa uwepo wa vitabu hivyo utasaidia kuinua ufaulu kwa wanafunzi kwenye masomo ya Sayansi  kwa sababu walikuwa na upungufu mkubwa wa vitabu hivyo.

“Vitabu hivi vitaleta mapinduzi makubwa katika ufundishaji na ufundishwaji  kwani mashuleni unakuta wanafunzi wana kitabu kimoja lakini wanaotumia ni wanafunzi kati ya watatu hadi watano,”alisema Mwl Tarimo.

Naye Mratibu wa Utalii wa Asili wa milima ya Chome na Shengena Elly Kimbwereza, ambaye alikuwa mwenyeji wa wageni hao, alieleza jinsi Utalii wa Asili unavyoweza kuunganishwa na shughuli za jamii husika na kuleta maendeleo .

Alisema uwepo wa vitabu hivyo vya masomo ya Sayansi vitasaidia katika sekta ya Tanzania ya viwanda  endapo wanafunzi hao watayasoma masomo ya Sanyansi wataweza kupatikana wataalam ambao wataweza kuendesha viwanda hapa nchi

0 Comments:

Post a Comment