Friday, August 23, 2019

UWT yafagilia uwekezaji wa JPM sekta ya Afya

Kaimu mganga mkuu hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mawenzi Josephine akipokea msaada kutoka kwa Makamu Mwenyekiti UWT Taifa Thuwaybah Kisasi  walipotembelea hospitali hiyo.


Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa (CCM) Taifa (UWT) Thuwaybah Kisasi, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa uwekezaji mkubwa aliouweka katika sekta ya afya nchini.

Kisasi, aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati wakati (UWT), walipoteembelea katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi, kwa lengo la kutoa misaada mbalimbali katika wodi ya wamama wajawazito pamoja na kutembelea mradi wa ujenzi wa jengo la ghorofa tatu la huduma ya afya ya mama na mtoto.

Kisasi alisema ameridhishwa na kazi kubwa ambayo  inaendelea kutolea katika hospitali ya rufaa ya mkoa Mawenzi na kuwataka watoa huduma za afya kuendelea kuwa wamoja, kupendana kila mtu na kuwataka kila mmoja kuendelea kutoa huduma kwa nafasi yake.

“Katika siku za nyuma, madaktari wengi walivunjika moyo wa kufanya kazi  kwa sababu kulikuwa hakuna vifaa, mazingira ya kufanyia kazi yalikuwa siyo mazuri, lakini kutokana na kuwepo kwa mabadiliko makubwa ya wamu ya tano tumeona kasi kubwa ya utendaji kazi katika nyanja mbalimbali,"alisema.

Aliongeza kusema kuwa “Naomba niwaeleze wazi nimeridhishwa sana na utendaji kazi wenu katika kuwahudimia wagonjwa, moyo  wa kufanya kazi tumerudishiwa na rais wetu Dkt. Magufuli,  sio hospitali tu bali  katika sekta zote,”alisema
Makamu mwenyekiti UWT Taifa Thuwaybah Kisasi akimpatia msaada wa mche wa sabuni.

Aidha Kisasi aliupongeza uongozi wa Manispaa ya Manispaa ya Moshi kwa jinsi unavyovutia kwa usafi ambao umeendelea kusifika nchini kote.

“Nimeelezwa kuwa mji huu umeendelea kuwa msafi kutokana na kutunga sheria ndogo ndogo za kusimamia usafi ambazo zimepelekea kuendelea kuongoza katika usafi kwenye Manipaa hapa nchini hongereni sana,” alisema Kisasi.

Kwa upande wake Katibu Mkuu (UWT) Taifa Mwl Queen Mlozi, alisema Wanawake ndiyo wanufaikaji wakubwa wa huduma za afya, hivyo, wanampongeza Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Magufuli kwa kasi kubwa ambayo anaendelea nayo ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ya Mwaka 2015/2020, katika huduma za jamii.

Awali akitoa taarifa ya hospitali hiyo Kaimu mganga mkuu Dkt. Josephine Rogath, alisema kuwa hospitali hiyo inakabiliwa na upungufu wa watumishi 232 wa kada mbalimbali.

“Hospitali haina kabisa madaktari bingwa wa dawa za usingizi, afisa utumishi, wataalam wa kada za wahudumu wa afya katika chumba cha kuhifadhia maiti, mtaalamu wa Tehama, fundi vifaa tiba, fundi sanifu wa dawa na fundi sanifu wa meno,"alisema Dkt. Rogath.

STORY BY: Kija Elias…..Agosti 22, 2019

3 comments: