Friday, May 31, 2019
ANNA DAVID: Maluweluwe yanavyotishia masomo yake
Anna David |
Mwanasaikolojia Gary Collins, raisi
wa zamani wa Washauri wa Chama Wakristu cha Marekani, aliulizwa uwezekano
kwamba maluweluwe yalikuwa kwa wafuasi na ndiyo yaliyobadili kwa kiasi kikubwa
tabia yao.
Collins alieleza, “Maluweluwe ni matukio ya mtu mmoja mmoja pekee” Kwa asili yake ni mtu mmoja peke yake anaweza kuona luweluwe fulani kwa wakati mmoja. Kwa hakika si vitu ambavyo vinaweza kuonwa na kikundi cha watu kwa wakati mmoja.” Hoja hiyo ya maluweluwe kuwa anaweza kuwa nayo mtu mmoja au wawili katika kundi kubwa la watu ikaungwa mkono na mwanasaikolojia Thomas J. Thorbum kwa kusema, “Haiingii akilini kabisa kwamba … watu mia tano, wenye akili timamu za kawaida wawe wameona aina zote za fahamu, za kuona, kusikia, kutenda – na kwamba zote hizi fahamu ziwe zimetokana na kuona maluweluwe – ndoto za mchana!”
Bado hoja ya maluweluwe kwa tafsiri ya wazungu iko hivyo kwa ulimwengu wa kiafrika imekaaje hiyo, mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka Mtwara Erick Thomas katika wimbo wake wa ‘Maluweluwe’ anatafsiri maluweluwe kuwa ni changamoto halisi za mwanadamu katika maisha, yaani mwanadamu anaona mambo katika hali ambayo ni tofauti na matarajio hali ambayo inamchanganya kabisa kufikia malengo.
Hata hivyo wasanii wengine wa kizazi kipya nchini Tanzania akiwamo Goodluck anajiuliza maluweluwe au ni ndumba (uchawi)? Mtumiaji mmoja wa mtandao wa intaneti anajiuliza nini hiki? “kataka kudaka mpira kaona moto, kataka kupiga mpira kaona paka, sasa sijui ndicho kilichotokea?..."
Bado hajapata jibu. Hapo ndipo kiini cha Makala haya ambayo yatamwangazia mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Sekondari ya Kikatoliki ya Visitation iliyopo Siha mkoani Kilimanjaro.
Anna David (16) amekuwa katika
changamoto kubwa hali ambayo imekuwa ikitishia masomo yake katika Shule ya
Sekondari ya Kikatoliki ya Visitation iliyopo Siha mkoani Kilimanjaro. Anna
alihamia shuleni hapo kwa nia ya kufanya vizuri katika masomo yake kutokana na
shule hiyo ya wasichana kuwa na msingi mzuri wa ufundishaji wa wanafunzi.
Anna anasema, “ Nilikubali uamuzi wa wazazi kunileta hapa lakini nimekuwa nikikutana na mambo magumu ndotoni, sijui ni nini hiki.” Aidha msichana huyo anasema hali hiyop inapomjia hujikuta akipiga kelele hivyo inatafsiriwa na walimu wa sekondari hiyo ya bweni kudhani kukiuka masharti ya shule.
Mwanafunzi huyo anasimulia kisa kimoja kilicholeta tafrani wakati bweni la shule hiyo lililoshika moto mwanzoni mwa mwaka huu. Anna anasema, “Moto uliwaka Jumamosi (siku hiyo bweni lilipokuwa likiungua)…nikawa namuona huyo moto kama kivuli, nikawa nawaambia watu wakawa wananiambia tusali na kuwa na Imani.”
Pia msichana huyo anasema, “Saa nyingine namuona kwenye ndoto…siku nyingine akaja usiku akanikaba.” Hata hivyo Anna anasema kuna mwanafunzi mwingine ambaye naye aliota kama yeye na akawatahadharisha wenzake kuwa kuna tukio litatokea.
“ Alituambia wiki hii haitaisha moto utawaka, mtoto huyo yuko form one (jina tunalihifadhi) lakini watu wakapuzia, tukapotezea huyo; siku hiyo ilikuwa jumamosi tulikuwa mimi na mtoto mwenzangu akaniambia njoo uone domu (bweni) la katikati linawaka moto,” anaongeza Anna.
Collins alieleza, “Maluweluwe ni matukio ya mtu mmoja mmoja pekee” Kwa asili yake ni mtu mmoja peke yake anaweza kuona luweluwe fulani kwa wakati mmoja. Kwa hakika si vitu ambavyo vinaweza kuonwa na kikundi cha watu kwa wakati mmoja.” Hoja hiyo ya maluweluwe kuwa anaweza kuwa nayo mtu mmoja au wawili katika kundi kubwa la watu ikaungwa mkono na mwanasaikolojia Thomas J. Thorbum kwa kusema, “Haiingii akilini kabisa kwamba … watu mia tano, wenye akili timamu za kawaida wawe wameona aina zote za fahamu, za kuona, kusikia, kutenda – na kwamba zote hizi fahamu ziwe zimetokana na kuona maluweluwe – ndoto za mchana!”
Bado hoja ya maluweluwe kwa tafsiri ya wazungu iko hivyo kwa ulimwengu wa kiafrika imekaaje hiyo, mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka Mtwara Erick Thomas katika wimbo wake wa ‘Maluweluwe’ anatafsiri maluweluwe kuwa ni changamoto halisi za mwanadamu katika maisha, yaani mwanadamu anaona mambo katika hali ambayo ni tofauti na matarajio hali ambayo inamchanganya kabisa kufikia malengo.
Hata hivyo wasanii wengine wa kizazi kipya nchini Tanzania akiwamo Goodluck anajiuliza maluweluwe au ni ndumba (uchawi)? Mtumiaji mmoja wa mtandao wa intaneti anajiuliza nini hiki? “kataka kudaka mpira kaona moto, kataka kupiga mpira kaona paka, sasa sijui ndicho kilichotokea?..."
Bado hajapata jibu. Hapo ndipo kiini cha Makala haya ambayo yatamwangazia mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Sekondari ya Kikatoliki ya Visitation iliyopo Siha mkoani Kilimanjaro.
Visitation Girls Secondary School, Siha; Kilimanjaro |
Anna anasema, “ Nilikubali uamuzi wa wazazi kunileta hapa lakini nimekuwa nikikutana na mambo magumu ndotoni, sijui ni nini hiki.” Aidha msichana huyo anasema hali hiyop inapomjia hujikuta akipiga kelele hivyo inatafsiriwa na walimu wa sekondari hiyo ya bweni kudhani kukiuka masharti ya shule.
Mwanafunzi huyo anasimulia kisa kimoja kilicholeta tafrani wakati bweni la shule hiyo lililoshika moto mwanzoni mwa mwaka huu. Anna anasema, “Moto uliwaka Jumamosi (siku hiyo bweni lilipokuwa likiungua)…nikawa namuona huyo moto kama kivuli, nikawa nawaambia watu wakawa wananiambia tusali na kuwa na Imani.”
Pia msichana huyo anasema, “Saa nyingine namuona kwenye ndoto…siku nyingine akaja usiku akanikaba.” Hata hivyo Anna anasema kuna mwanafunzi mwingine ambaye naye aliota kama yeye na akawatahadharisha wenzake kuwa kuna tukio litatokea.
“ Alituambia wiki hii haitaisha moto utawaka, mtoto huyo yuko form one (jina tunalihifadhi) lakini watu wakapuzia, tukapotezea huyo; siku hiyo ilikuwa jumamosi tulikuwa mimi na mtoto mwenzangu akaniambia njoo uone domu (bweni) la katikati linawaka moto,” anaongeza Anna.
Sophia ambaye ni mama mdogo wa Anna David akizungumza na JaizmelaNews. |
Kwa upande wa mama mdogo wake ambaye
alijitambulisha kwa jina la Sophia, alisema waliitwa shuleni mara mbili
kutokana na tabia ya ghafla iliyojitokeza ya kupiga makelele. “Tuliambiwa kuwa
Anna anapiga makelele anawafanya wenzie wasisome, anawasumbua kwa
ujumla..ikabidi tufike shuleni na kumchukua,” alisema Sophia.
Sophia anasema
baada ya kutoka naye shuleni walikwenda naye katika nyumba za ibada kwa ajili
ya maombi kwani katika maisha yake tangu amezaliwa hawajawahi kumuona
akisumbuliwa na hali hiyo. Aidha mama mdogo huyo anasema kabla hawajamrudisha
shuleni wakapigiwa simu kutoka shuleni kuwa binti yao anahusika na uchomaji wa
bweni.
“Tukaamua tumpeleke kwenye maombi, akapata matibabu kabla hajapona
tukapigiwa simu kuwa kuna kikao baada ya kufika tukaambiwa kuwa Anna hatakiwa
kwani ndiye aliyechoma mabweni,” anaongeza Sophia.
Hata hivyo familia ya binti huyo wa kidato
cha kwanza inadhamiria kumuondoa shuleni hapo kutokana na changamoto hiyo
ifikapo mwezi wa saba.
Mbali na hali hiyo makala haya yalimtafuta Mhubiri wa
Injili Zakaria Misitu ambaye alisema, “ Mtu anapotokewa na hali hiyo, cha
kwanza ni kumfanyia maombi kwani hakuna linaloshindikana kwa Mungu na pia
ushauri nasaha unapaswa kuendelea kufanywa kwa mtu wa jinsi hiyo ili roho chafu
zisiweze kumrudia.”
Geti la kuingilia la Visitation Girls Secondary School. |
Thursday, May 30, 2019
MAKTABA YA JAIZMELA: Jonas Savimbi 1934-2002
Jonas Malheiro Savimbi ni moja ya wanasiasa
na Wapigania Uhuru katika moja ya mataifa yaliyopo kusini mwa Afrika yaani
Angola. Aliuawa kinyama Februari 2002 kwa kumiminiwa Risasi na vikosi vya jeshi
la Angola.
Sasa ni miaka 17 mzozo umeibuka baina ya serikali ya Angola na
upinzani juu ya mipango ya kuzika upya mwili wa aliyekuwa kiongozi wa vugugu la
waasi wa Unita ambaye kifo chake kilitokea miaka 17 iliyopita na kumaliza vita
vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa takribani miongo mitatu.
Serikali ilikuwa inataka kuukabidhi mwili wa Savimbi kwa wawakilishi wa Unita, ambacho sasa ni chama cha upinzani, ili waweze kuuzika mwili wake nyumbani kwao Juni Mosi mwaka huu. Hata hivyo, makabidhiano ya mwili hayakufanyika na kila upande sasa unamlaumu mwingine. Helena Savimbi, mmoja wa watoto wa kike wa kiongozi huyo wa waasi ameliambia shirika la habari la AFP kwamba serikali haikuheshimu mkataba.
Serikali nayo imeishutumu Unita kwa kushindwa kuuchukua mwili Jumanne, kama walivyokubaliana. Kikiwa ndio chama kikuu cha upinzani , Unita kimekuwa kikifanya kampeni ya kutaka mwili wa Savimbi uzikwe kwa heshima. Mwili wake uliofukuliwa ulitakiwa kukabidhiwa na serikali kwa Unita siku ya Jumanne. Jonas Savimbi ni nani katika ardhi ya Taifa la Angola na nje? Fuatana nami katika makala haya.

Jonas Savimbi alizaliwa Agosti
3,1934 katika eneo linalojulikana kama Munhango Jimboni Bie Angola wakati
wakoloni wa Kireno wakilitawala Taifa hilo. Kwa miaka zaidi ya 30 Savimbi alipigana
msituni hii inamfanya kuonekana mpiganaji hodari wa vita vya msituni. Aliuawa
kinyama karibu na Lucusse katika jimbo la Moxico nchini Angola. Jonas Savimbi alikuwa
ni mwanasiasa na kiongozi wa muda mrefu Wa Kikosi cha Askari wapigania Uhuru Wa
Msituni. Angola ni moja ya mataifa yaliyojinyakulia uhuru kwa mtutu wa bunduki
ikisaidiwa na mataifa yaliyokuwa mstari wa mbele (Frontline States) kama
Tanzania , Zimbabwe n.k .
Jonas Savimbi alipigania Uhuru kutoka kwa Wakoloni wa Kireno na baada ya Uhuru Wa Angola mwaka 1975 yeye aliendelea kupigana na Serikali ya Angola kwani katika fikra zake aliamini bado watu wa Angola hawajapata Uhuru kamili.

Kihistoria yeye ni mtoto Wa
Mfanyakazi wa Reli ya Benguela ,Alikuwa ni Mkuu wa kituo cha Reli. Kitaaluma alisoma
katika shule za kidini za misheni ambazo kwa wakati huo zilikuwa ngumu sana
Kuwapokea watu weusi kutokana na moja ya ndugu yake Savimbi kuwa moja ya
machifu Wa kabila la Ovimbundu basi ikawa rahisi kufanya Urafiki na
wamishionari Wa Roman katoliki na kufanikiwa kuhitimu masomo yake ya awali na
baadaye alipata ufadhili wa kimasomo na kwenda ng'ambo (Ulaya). Savimbi alisoma
taaluma ya Madawa(Udaktari) katika chuo kikuu cha Lisbon nchini Ureno mnamo
mwaka 1958-1960, Chuo Kikuu cha Fribourg mwaka 1961- 1964 na baadaye alijiunga
na chuo kikuu cha Lausanne nchini Uswisi huku akibobea katika Sayansi ya Siasa
mnamo mwaka 1964-1965.
Huku akiwa masomoni huko Lisbon miaka ya 1950 alianza kuupinga utawala katili wa Kireno nchini Angola. Mnamo mwaka 1961 Savimbi alipata kiu kubwa sana na kuamua kufanya harakati za kulikomboa Taifa la Angola kutoka katika makucha ya wakoloni Wa Kireno hivyo akajiunga na moja ya kundi la wapigania Uhuru lijulikanalo kama Popular Union of Angola (UPA). Baadaye National Liberation Front Of Angola (FNLA) lililokuwa chini ya Uongozi wa Holden Roberto. Alijiunga kama mpiganaji wa kawaida asiye na ujuzi mkubwa katika mapambano ya Msituni.
Mnamo mwaka 1965 alipata nafasi ya kwenda nchini China na kupata mafunzo makubwa ya kijeshi akibobea Katika mapambano ya vita vya msituni (Guerrilla war) .Mwaka huo alikutana na kiongozi wa Taifa la Uchina Mao Tse Tung ,Viongozi wa Kijeshi na wanasiasa wa chama cha Kikomunisti ambao wote kwa pamoja walimpa mbinu mbalimbali za kukabiliana ktk vita vya Msituni. Savimbi aliwahi kaririwa na Gazeti la Reader's Digest akisema " Kutoka kwa Mao na Wakomunisti nilijifunza namna ya kupigana na kushinda Vita vya Msituni.
Lakini vilevile nilijifunza kuendesha Uchumi au Taifa ,Utajiri Wa Taifa hutengenezwa na hatua zinazochukuliwa na watu Binafsi ". Baada ya mafunzo ya kijeshi huko China Savimbi alirejea nyumbani na kuendeleza harakati zake za ukombozi wa Taifa la Angola . Aliporudi alianza taratibu kuwahamasisha watu Wa jamii ya Ovimbundu ambao ni robo tatu ya nchi hiyo kuanza kujitambua na kupigania Uhuru wao kutoka kwa Mkoloni wa kireno.
Mnamo Machi 13, 1966 Baada ya kuona kundi la FNLA ni dhaifu sana halifikii malengo yake aliamua kujiengua au kujitoa na kuunda kundi la wapigania uhuru lijulikanalo kama National Union for the Total Independence of Angola (UNITA) na kuanza kuendeleza ndoto yake ya kuung'oa utawala Wa Kireno .Udhaifu Wa FNLA ulitokana na mapigano yake dhidi ya watawala Wa Kireno kuanzia nchini Zaire kwa sasa DRC. Kutokana na sababu FNLA walikuwa dhaifu sana na kiu yake Savimbi ilikuwa ni kuanzisha mapambano kutokea ktk Ardhi ya Angola Siyo Zaire (DRC).Savimbi alishirikiana na Antonio da Costa Fernandez kuliunda kundi la UNITA ktk Eneo lijulikanalo kama Muangai kwenye jimbo la Moxico.
Mnamo Disemba 25,1966 pambano la Kwanza La UNITA lilifanywa dhidi ya Wakoloni Wa Kireno. Savimbi ndiye kiongozi wa wapiganaji Wa Msituni aliyesalia nchini Angola huku akipigana na Wareno kwani alikuwa amejiamini vilivyo dhidi ya utawala katili na dhalimu Wa Wareno .Mnamo Novemba 10,1975 Taifa la Angola lilipata Uhuru wake kutoka kwa Wareno. Hatimaye Harakati za kutaka kuunda Serikali huru ya Angola zikaanza na chama cha MPLA kikiwa ni miongoni mwa vyama vilivyokuwa vikipigania Uhuru dhidi ya Wareno kiliunda Serikali mpya.

Savimbi kama miongoni mwa wapiganiaji Wa Uhuru Wa Angola hakuridhishwa na ugawanaji Wa madaraka na hatimaye kuapa kupambana kwa njia ya vita vya Msituni mpaka atakapotwaa madaraka na kuiangusha MPLA .Kilichomuudhi sana Savimbi kitendo cha Wareno kukipa mamlaka chama cha MPLA kuunda Serikali mpya ambayo itakuwa inafuata misingi zaidi ya kijamaa huku washirika wake wakubwa hasa Marekani wakiwa ni waumini Wa Sera za kibepari.
Savimbi alipenda uchumi Wa Soko huria ambao kila mtu anakuwa huru kumiliki Ardhi ,Biashara na Viwanda. Savimbi aliingia Msituni na kusababisha Serikali ya Chama Tawala -MPLA kuomba msaada wa kijeshi kutoka nchini Cuba na Urusi ambapo haikuchukua muda sana vikosi vya majeshi ya Cuba na Urusi vilianza kujipenyeza nchini Angola kwa njia mbalimbali ikiwemo njia ya maji ,Ardhini na Angani .Majeshi ya Cuba na Urusi yakiwa na hamasa kubwa sana ya kutaka kuulinda ukoministi nchini Angola yalitumia nguvu kubwa sana kupambana na Vikosi vya kijeshi vya Savimbi vilivyokuwa vikipokea mafunzo ya Hali ya juu kutoka kwa jeshi la Marekani. Savimbi akiwa Msituni alinusurika Mara kadhaa kuuawa lakini vikosi vya Marekani vilivyoingia kwa siri nchini Angola vilimuokoa kutokana uhodari wa vikosi hivyo.
Hadi mwaka 1975 Jonas Savimbi alikuwa ameongeza wafuasi wengi wa msituni huku akiwa na dhamira ya dhati ya kuchukua udhibiti kamili Wa nchi hiyo .UNITA kwa sehemu kubwa ilijikita katika maeneo makubwa ya Kusini -Mashariki ya nchi hiyo na Asilimia kubwa Savimbi alipata uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa watu Wa Jamii ya Ovimbundu na ndio Wengi sana nchini Angola. Kikosi kikubwa cha wapiganaji wa Savimbi kilitokana na watu jamii ya Ovimbundu.
Je, Jonas Savimbi alipata wapi msaada kiwango cha kutikisa Serikali ya Kikoloni ya Ureno na Hatimaye Serikali ya MPLA baada ya Uhuru? Kiufupi Mwanasiasa na mpiganaji huyu Wa Msituni alipokea msaada Wa Silaha, Mavazi ya kijeshi, Chakula, Madawa kutoka kwa nchi ya China, Afrika kusini na Marekani wakati Serikali ya Angola chini ya chama Tawala -MPLA ikisaidiwa na uliokuwa muungano Wa Urusi (USSR). Marekani ilikuwa ikihamasisha Serikali za Zambia, Israel, Bulgaria, Saudi Arabia, Zaire (DRC), Morocco, Ufaransa ili kuwasaidia wapiganaji Wa UNITA. Savimbi alipokea msaada mkubwa kutoka kwa marais kadhaa Wa Marekani akiwemo Ronald Reagan kuna wakati Gazeti la Marekani la Washington Post lilimnukuu akisema "Savimbi ni mpigania Uhuru ambaye anapambana kuvitoa Vikosi vya Kijeshi vya Serikali ya Cuba na Muungano Wa Urusi kutoka nchini Angola". Katika utawala wa Rais Reagan inadaiwa Savimbi alikuwa akipokea msaada wa kifedha hadi Dola millioni 15 ($15million ) na Silaha za kupambana na Ndege vita na makombora ya Urusi.
Savimbi alipata marafiki wengi sana nchini Marekani na wengi walimwamini na kumpa msaada ili kuuondoa utawala wa Kireno na baadaye utawala wa chama Tawala MPLA chini ya Rais José Eduardo dos Santos. Utawala wa Santos kwa wamarekani waliona kama ni wakidikteta .Katika Harakati zake bwana Savimbi alishutumiwa vikali na mashirika ya haki za Binadamu Barani Afrika na Duniani hasa Kutokana na mbinu zake za kukabiliana na vikosi vya Serikali ya Angola vikisaidiwa na Cuba na Urusi.
Mkurugenzi mmoja Wa Shirika la haki za Binadamu ajulikanaye kama Rakiya Omaar hapa Afrika alivishutumu vikali vikosi vya Bwana Savimbi .Omaar alinukuliwa akisema " Shirika la Haki za Binadamu hapa Afrika limebaini kuwa Lengo la UNITA ni kutisha watu ili waiunge mkono au kuwaadhibu kwa sababu wanaunga mkono majeshi ya Serikali " .Mashariki mwa Angola ,Mbinu nyingi za UNITA zililenga kuwafanya Raia wateseke na njaa kwa kuchoma mazao ktk mashamba mengi huku ikizuia misaada ya kibidamu kutoka umoja Wa mataifa na Afrika.
Mnamo miaka ya 1970 na 1980 Savimbi aliendelea na mapambano makali ya vita dhidi ya Serikali ya Chama Tawala -MPLA .Haikuwa rahisi kumpiga Savimbi .Mawazo yake ya kuitawala Angola yalikuwa sana kwa kasi ndani na nje ya mipaka ya Taifa hilo Tajiri kwa mafuta ,Dhahabu na madini ya chuma .Mawazo ya Savimbi yalikuwa ni Kutengeneza Uchumi Wa Soko Huria ,Uchaguzi Wa vipindi na mabadiliko makubwa ya katiba ya Angola.
Savimbi alimchukulia Rais José Eduardo dos Santos kuwa ni dikteta kwani kwa muda mrefu Angola baada ya Uhuru haikuwa na Uchaguzi Wa vyama vingi. Mwaka 1991 vikosi vya Jonas Savimbi vilingia mji Mkuu Luanda na kuudhibiti vikali ambapo umeme na miundo mbinu yake viliharibiwa vibaya sana, Barabara yakiwemo madaraja yalivunjwa ,Reli iliharibiwa vibaya na hatimaye gharama takribani dola billioni 20 zilitumika kurejesha miundo mbinu hiyo muhimu. Taifa liliingia katika deni kubwa pasipokutarajia na hivyo hatua kadhaa za kuleta amani zilianza kuchukuliwa kwa maslahi ya watu wote wa Angola.
Baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa zaidi ya muongo mmoja Mei 30,1991 Savimbi alikubali na kusaini mkataba na chama Tawala -MPLA hatimaye Amani ilirejea na kisha uchaguzi wa mfumo Wa vyama Vingi uliitishwa mwaka 1992 ambapo chama cha UNITA kupitia Savimbi kilianza kufanya kampeni za Uchaguzi .Savimbi aligombea Kama Rais kupitia chama cha UNITA .Savimbi ktk kampeni za Urais aliahidi Kuhakikisha uchaguzi kufanyika kwa vipindi tofauti na awali ambapo hakukuwa na uchaguzi wa kdemokrasia ,watu kumiliki Ardhi ,Watu kumiliki Biashara na Uwepo wa Soko Huria nchini Angola.
Katika uchaguzi mkuu huo Savimbi alinukuliwa mbele ya Umati mkubwa wa watu Jijini Luanda akisema "Nguvu ya UNITA haipimwi kwa Majeshi yake bali ni kwa Uwepo wake Kisiasa " Ktk Uchaguzi huu Chama cha MPLA kikiongozwa na Rais José Eduardo dos Santos killibuka kidedea maeneo mengi ya nchi hiyo . Baada ya Uchaguzi huu bwana Savimbi hakuridhika na matokeo akidai uchaguzi uligubikwa na udanganyifu ndipo UNITA ilirudi Msituni ili kutaka kuitawala nchi hiyo ambapo vita vya wenyewe kwa wenyewe vilizuka upya tena na kusababisha kwa kiwango kikubwa maeneo ya vijijini kudhibitiwa na kuwa chini ya Wapiganaji Wa Bwana Savimbi .Maefu ya watu walikufa na kujeruhiwa vibaya ,Visa vya ubakaji vilishamiri ,Njaa kubwa ilitokea ,Miundo mbinu kama Reli, Barabara, Madaraja yalivunjwa ,Viwanda viliripuliwa n.k .Vilikuwa ni vita vibaya sana kuwahi kutokea kusini mwa Afrika.
Baada ya mapigano makali na yasiyoisha mnamo mwaka 1994 mazungumzo ya Amani yalifanyika mjini Lusaka -Zambia ambapo mahasimu walikutana na kukubaliana kushusha chini Silaha na kuviamrisha vikosi vyao vya wapiganaji kuondoka kwenye baadhi ya maeneo ili kurahisisha mapatano. Katika makubaliano ya pande mbili Aliyekuwa Rais Wa Angola ndugu José Eduardo dos Santos alikubali kutoa nafasi mbili za umakamu wa Rais kwa UNITA hatimaye Serikali ya pande mbili ikaundwa. Mwaka 1997 Savimbi alijiuzulu nafasi hiyo na Hatimaye Serikali ya Angola ilimrejesha ktk nafasi hiyo mwaka 1998. Mwaka 1996 ilidaiwa kwamba Jonas Savimbi Alikuwa na harakati za kuchukua udhibiti Wa Eneo la kaskazini-Mashariki ambalo lilikuwa linautajiri mkubwa Wa madini ya Dhahabu ,Wapiganaji wake walidhibitiwa na kupewa kazi jeshini hatimaye mpasuko mkubwa ukaanza kujitokeza ndani ya UNITA.
Marekani ilikuwa ikibeba utajiri mkubwa wa Dhahabu ktk Eneo hili ndio maana ilikuwa ikitoa Msaada mkubwa Wa kijeshi ili kulinda masirahi yake .Baada ya vikosi vya Serikali kulidhibiti Eneo hili Marekani ilipunguza msaada Wa Silaha na hatimaye nguvu ya Savimbi ilipungua kwa kiwango kikubwa ingawaje aliendelea kuwa imara dhidi ya Serikali ya José Eduardo dos Santos . Septemba mwaka 1998 Savimbi alikutana na upinzani mkali sana ndani ya UNITA hatimaye kundi jingine lililojiita UNITA-R lilijitokeza na kujitangazia uongozi wake.
Tangu hapo ndipo ukawa mwanzo wa kutokea makundi matatu ndani ya UNITA. Kutokana na mgawanyiko huo Serikali ya Angola na Jumuiya ya Maendeleo kusini Mwa Afrika (SADC) walilitambua kundi la UNITA-R kama kundi rasmi linaloiwakilisha UNITA. Kwenye miaka ya 2000 Marekani ulikuwa imethibitisha kwa asilimia kubwa misaada yake ya kijeshi kwa Jonas Malheiro Savimbi kwani hakuna faida yoyote ambayo wamarekani walikuwa wanaipata kutoka kwake ikiwa migodi iliyokuwa inadhibitiwa na wapiganaji Wa Savimbi ilikuwa imetwaliwa na jeshi la Angola. UNITA ilipoteza Rasilimali kubwa kutoka nje hasa baada ya Kutwaliwa migodi ile ilyokuwa ikiwaingizia fedha za magendo uliowasaidia kupata Silaha nyingi na za kisasa kwa ajili ya kuendesha mapambano dhidi ya Serikali.
Mwaka 2001 Jonas Savimbi hatimaye kwa hiari yake alikubali mkataba Wa Amani wa Lusaka -Zambia uliosainiwa na pande mbili ili kuleta Amani .Wakati Serikali ikitaka usimamishaji wa vita na UNITA, Savimbi alilitaka kanisa la Roman katoliki ndilo liwe msuluhishaji Wa Mgogoro ule lakini mapigano makali yaliendelea mwaka mzima hatimaye kuvuka mipaka na kuingia nchini Zambia na Namibia. Majeshi ya Serikali ya Angola yaliendelea kumfuatilia Savimbi na vikosi vyake mpaka walipofanikiwa kumkamata Mashariki mwa jimbo la Moxico na Hatimaye kumminia Risasi nyingi sana mwilini mwake na hatimaye kupoteza maisha yake mnamo Februari 22, 2002. Baada ya Jonas Savimbi kuuawa makubaliano ya Amani yalisainiwa kati ya UNITA na Serikali ya Angola hapo Mwezi Aprili 2002.
Balozi wa Sweden awataka Wanachama wa Klabu za Waandishi wa habari kubuni miradi
Balozi wa Sweden nchini Tanzania Anders Sjoberg amewataka Wanachama wa Klabu za Waandishi wa habari hapa nchini kubuni miradi mikubwa itakayo wainua kiuchumi na kuacha kuendelea kuwategemea wafadhili pekee.
Balozi Sjoberg, aliyasema hayo jana wakati wa ziara yake mkoani Kilimanjaro, yenye lengo la kujionea shughuli za Klabu ya waandishi wa habari mkoani humo, jinsi inavyojiendesha, ambapo alisomewa taarifa ya Klabu hiyo na Katibu wa (MECKI) Nakajumo James.
Balozi Sjoberg, aliwataka Wanachama wa Klabu za Waandishi wa habari kote nchini kutafuta miradi ambayo italenga kuwainua kiuchumi na kuwasaidia wanahabari bila kuvunja sheria za nchi.
“Lengo kubwa la ziara yangu iliyonisukuma kufika katika Klabu yenu ya MECKI, ni kutaka kufahamu mazingira halisi ya ufanyaji kazi wa waandishi wa habari pamoja na kupata maoni juu ya sheria ya huduma ya vyombo vya habari ya mwaka 2016,”alisema.
Aliongeza kuwa “Napenda niwapongeze Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Kiliamnjaro kwanza kwa taarifa yenu nzuri, ila napenda niwape changamoto kwenu ni vyema sasa mkaanza kufikiria kuwa na miradi yenu ya Klabu ambayo italenga kuwainua kiuchumi na kuwasaidia wanahabari bila kuvunja sheria za nchi.,”alisema Sjoberg.
Akitolea mfano wa miradi ambayo kama Klabu inaweza kuianzisha ni miradi ya masuala ya Afya na Elimu, ambayo ni maeneo muhimu sana katika jamii, na miradi hiyo iwe ya miaka mitano, Klabu zitafute wafadhili na kuacha kutegemea chanzo kimoja tu, hicho hakiwezi kuwa kwamua kiuchumi.
Vilevile Balozi Sjoberg, alisema miradi kama hiyo itaweza kuwapatia fedha nyingi ambazo zitawawezesha kuendesha Klabu pamoja na maisha ya kiuchumi ya waandishi wa habari ambao ni wanachama wa Klabu tu, ambao ndio watakuwa wanufaika na wasimamizi wa miradi hiyo.
“Waandishi wa habari mnazo fursa nyingi sana za kiuchumi, lakini hamtaki kuzitumia fursa hizo kwa mfano Klabu ya MECKI, mnaweza kuanza na mradi wa masuala ya Afya, ama Elimu wa miaka mitano mkaandika andiko lenu, wafadhili wapo tu, mtapata fedha nyingi na zitaweza kupunguza ukali wa maisha, lakini pia itawezesha kuwavutia hata waandishi ambao sio wanachama wavutiwe kujiunga na Klabu yenu,”alisema.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Kilimanjaro MECKI, Bahati Mstapha alimweleza Balozi huyo, changamoto kubwa inayowafanya wanahabari wengi kutokujiunga na Klabu yao ni uwepo wa ada kubwa jambo ambalo limewafanya waandishi wengi kutokujiunga na Klabu hiyo.
“Sisi kama Klabu ya MECKI tunajiendesha kwa utaratibu wa chini ya mwamvuli wa UTPC, kupitia mpango kazi wa mwaka 2016/2020 kama matakwa ya mfadhili yanavyotutaka,”alisema Mstapha.
Aidha Mwenyekiti wa Klabu hiyo Bahati Mstapha, alimuomba Balozi huyo kuwapatia wanachama wa Klabu ya MECKI ziara ya kwenda nchini Sweden kwa lengo la kubadilishana uzoefu na waandishi wa habari nchini humo jinsi wanavyo fanya kazi, ambapo Balozi huyo alisema ni wazo zuri ambalo atalifanyia kazi na atawapatia majibu
Wednesday, May 29, 2019
Jela mwezi mmoja kwa kutelekeza familia
Mwanaume mmoja mjini Moshi mkoani
Kilimanjaro amehukumiwa jela mwezi mmoja kwa kosa la kuitelekeza familia yake.
Mahakama ya Mwanzo mjini Moshi
imemhukumu kifungo cha mwezi mmoja jela Mokolo Anselim Tengecha (37) kwa kosa
la kuitelekeza familia yake.
Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mwanzo
mjini Moshi Adnan Kingazi alisema mshtakiwa alikiuka kukiuka kifungu cha 166
cha makosa ya jina sura ya 16 ya kanuni ya adhabu.
Awali ilidaiwa mahakamani hapo kuwa
tarehe 10 Machi 2018 mshtakiwa akiwa
katika maeneo ya Matindigani, Pasua bila halali na huku akijua kufanya hivyo ni
kosa alimtelekeza mkewe anayefahamika kwa jina Zaina Mustapha Makame (22) akiwa
na mtoto wake Omary Said (6) na Shaban Said (Mwaka mmoja na miezi tisa) bila
kuwapa chochote na kutokomea kusikojulikana.
Aidha ilidaiwa mahakamani hapo kuwa
mshtakiwa alitafutwa kwa miezi kadhaa bila kuonekana na baada ikabainika kwamba
alikuwa amepanga chumba kingine katika mtaa mwingine hapo hapo Matindigani na
kuishi na mwanamke mwingine.
Ilidaiwa mahakamani hapo kutokana na
kushindwa kulipa pango la nyumba mama mpangaji alimtimua mlalamikaji kwa kumtupia
virago nje hali iliyomlazimu mlalamikaji kulala nje kwa mateso akiwa na watoto
wake wawili.
Upande wa mashtaka uliieleza mahakama
kuwa mshtakiwa ni mtu anayejishughulisha na kupandisha watalii katika mlima Kilimanjaro.
Aidha ilielezwa ushahidi uliotolewa
na upande wa mashtaka mahakama iliona ni mzito. Kwa upande wake mshtakiwa
alipotakiwa kujitetea kwanini mahakama isimpe adhabu mshtakiwa alisema haoni
haja ya kujitetea ndipo Mahakama ilimpomtupa jela mwezi mmoja ili iwe fundisho
kwa watu wenye tabia kama hizo.
MAKTABA YA JAIZMELA: Rais wa 35 wa Marekani John Fitzgerald Kennedy
John
Fitzgerald "Jack" Kennedy alizaliwa Mei 29, 1917 na kuuawa Novemba 22, 1963), alikuwa akijulikana kwa
kifupi kama JFK.
JFK alikuwa mwanasiasa wa Marekani aliyekuwa rais wa 35 wa
Marekani tangu Januari 1961 hadi kuuawa mwezi Novemba 1963. Alihudumu kwa wakati
wa vita baridi. Katika utawala wake alihusika kusimamia uhusiano na Urusi
wakati huo USSR. JFK aliingia madaraka kwa tiketi ya Chama cha Democratic.
Alianza mbio za kuingia White House ya Washington D.C akianza katika Baraza la Wawakilishi akitokea
Massachussets na baadaye Seneti nchini humo. JFK alizaliwa Brookline,
Massachusetts na alihitimu Chuo Kikuu cha Harvard mwaka 1940 kabla ya kujiunga
na U.S. Naval Reserve mwaka uliofuata.
Wakati wa Vita Kuu ya II, alisimamia
mapambano ya majini katika boti za PT kwenye bahari ya Pasifiki na alipata
Medali ya Navy na Marine Corps kwa ajili ya huduma yake. Baada ya vita, Kennedy
aliwakilisha wilaya ya 11 akitokea Massachusetts katika Baraza la Wawakilishi la
Marekani kutoka mwaka wa 1947 hadi 1953.
Alichaguliwa kwa Seneti ya Marekani na
akahudumu kama Seneta mdogo kutoka Massachusetts tangu 1953 hadi 1960. Wakati
akiwa Seneta, alichapisha kitabu chake “Profiles in Courage”, ambacho kilipata
Tuzo ya Pulitzer kwa Wasifu. Katika uchaguzi wa rais wa 1960, Kennedy alimshinda
mshindi wa Republican Richard Nixon, ambaye alikuwa makamu wa rais. Alipokuwa
na umri wa miaka 43, akawa mtu wa pili mdogo zaidi kutumikia kama rais, mtu
mdogo sana aliyechaguliwa kuwa rais wa U.S.
Pia aliweka rekodi ya kuwa rais wa
kwanza muumini wa kanisa katoliki kukalia kiti
kama haitoshi alikuwa rais wa kwanza kuhudumu katika Jeshi la Majini la
Umoja wa Mataifa. Wakati wa Kennedy
katika ofisi kulikuwa na mvutano mkubwa
na nchi za Kikomunisti katika Vita Baridi.
JFK aliongeza idadi ya washauri wa
kijeshi kwa ajili ya Vietnam Kusini Ikikumbukwe kwamba JFK alipokea mikoba
kutoka kwa Dwight D. Eisenhower. Mnamo Aprili 1961, aliidhinisha jaribio la
pamoja la CIA ambalo lilishindwa kuipindua serikali ya Cuba ya Fidel Castro.
Hatimaye alikataa mipango ya Operesheni Northwoods na
Wafanyakazi wa Pamoja ili kuondokana na mashambulizi ya bendera ya uongo juu ya
udongo wa Marekani ili kupata uungwaji mkono kutoka kwa wananchi wa Marekani
juu ya vita dhidi ya Cuba. Hata hivyo utawala wake uliendelea kupanga mpango wa
uvamizi wa Cuba katika majira ya joto ya 1962.
Mnamo Oktoba 1962, ndege za kijasusi za Marekani ziligundua kuwa hazina ya zana kubwa za kivita zilizopelekwa na Urusi katika ardhi ya Cuba. Katika hilo kukazuka ugomvi wa siku 13 ambao uliwahusisha Marekani na Urusi aliyekuwa nyumba ya Cuba. Baada ya mapigano hayo mataifa hayo yalifikia makubaliano waliyotiliana saini. Ndani ya nchi, JFK aliongoza juu ya uanzishwaji wa Peace Corps na kuunga mkono harakati za haki za kiraia, lakini ilifanikiwa tu katika kupitisha sera zake za ndani za Frontier.

JFK WAKATI WA UTOTO
JFK alizaliwa kwa baba
yake aliyekuwa mfanyabiashara na mawanasiasa Joseph Patrick ‘Joe’ Kennedy huku
mama yake Rose Elizabeth Fitzgerald Kennedy
akiwa ni mtoaji wa huduma mbalimbali katika jamii. Baba yake P.J Kennedy
alikuwa mwananchama wa bunge la serikali Massachussets.
Wazazi wote wanne walikuwa watoto wa wahamiaji wa Ireland. JFK aliishi Brookline kwa miaka kumi ya kwanza ya maisha yake na alikuwa akisali katika Kanisa la St. Aidan, ambako alibatizwa mnamo Juni 19, 1917. Alisoma katika Shule ya Devotion Edward huko Brookline, pia Noble na Greenough karibu na Dedham, Massachusetts, JKF alikwenda tena katika shule ya Dexter nayo ikiwa katika Brookline.
Mnamo Septemba 1931, JFK alikimbilia Connecticut katika shule ya Choate pale Wallingford. Wakati wa miaka yake katika Choate, JFK alikuwa na matatizo ya afya ambayo ilisababisha kupelekwa hospitalini hii ilikuwa mwaka 1934. Madaktari wa Hospitali ya New Haven, walidhani JFK angeweza kuwa na leukemia.
Lakini baadaye ilikuja kujulikana kuwa sio Leukemi. Hiyo iligunduliwa baada ya juhudi za madaktari wa Kliniki ya Mayo huko Rochester, Minnesota. Mnamo Septemba 1935,JFK alifanya safari yake ya kwanza nje ya nchi wakati alipokuwa akienda London na wazazi wake na dada yake Kathleen. Septemba 1936, JFK alijiunga na Chuo cha Harvard, katika maombi yake ya kujiunga na chuo hicho alisema; "Sababu nilizo nazo za kuchagua Harvard ni nyingi.
Harvard inaweza kunipa historia bora na elimu bora zaidi kuliko chuo kikuu chochote Nimekuwa nilitaka kwenda huko.” Mwaka 1939 JFK alizunguka Ulaya, Umoja wa Kisovieti, Balkans, na Mashariki ya Kati katika maandalizi ya Thesis ya heshima ya Chuo cha Harvard. Kisha akaenda Czechoslovakia na Ujerumani kabla ya kurudi London mnamo Septemba 1, 1939, siku ambayo Ujerumani ilivamia Poland kuashiria mwanzo wa Vita Kuu ya II.
Siku mbili baadaye, familia hiyo ilikuwa katika Baraza la Wakuu kwa mazungumzo ya kuidhinisha tamko la Uingereza la vita dhidi ya Ujerumani. Mnamo mwaka wa 1940 JFK aliingia Jeshi, lakini alikuwa na afya ya kutosha kutokana na matatizo yake ya chini ya nyuma. JFK aliapa kama Rais wa 35 saa sita mchana Januari 20, 1961. Katika anwani yake ya kuanzisha, alizungumza juu ya haja ya Wamarekani wote kuwa raia wenye nguvu, na kusema kwa bidii: "Usiulize ni nini nchi yako inaweza kukufanyia, waulize unachoweza kufanya kwa nchi yako. "
Aliwaambia mataifa ya dunia kujiunga na kupambana na kile alichoita "maadui wa kawaida wa mtu: udhalimu, umaskini, magonjwa, na vita yenyewe." Akiwa Rais katika iKulu ya Marekani JFK alileta tofauti kubwa ukilinganisha na mtangulizi wake Eisenhower, na hakuwa na muda wa kukataa njia za Eisenhower. JFK alikuwa tayari kufanya maamuzi ya haraka yaliyotakiwa katika mazingira kama hayo. Alichagua mchanganyiko wa watu wenye ujuzi na wasiokuwa na uzoefu wa kutumikia katika baraza lake la mawaziri. "Tunaweza kujifunza kazi zetu pamoja", alisema JFK.
Kwa kiasi kikubwa cha washauri wake wa kiuchumi, ambao walitaka kupunguza kodi, JFK alikubaliana nao haraka ahadi ya bajeti ya usawa.

KUUAWA KWA JFK
Rais Kennedy aliuawa huko Dallas, Texas, saa 12:30 jioni
Central Standard Time siku ya Ijumaa, Novemba 22, 1963. Alikuwa Texas akiwa na
safari ya kisiasa. Alipokuwa akiendesha gari la rais katika jiji la Dallas,
alipigwa mara moja nyuma, risasi ikitoka kwenye koo yake, na mara moja katika
kichwa.
JFK alipelekwa Hospitali ya Parkland kwa ajili ya matibabu ya dharura, ambako alitamkwa kuwa amekufa baada ya dakika 30 baadaye. Alikuwa na umri wa miaka 46 na alihudumu Wiite House kwa siku 1,036. Lee Harvey Oswald muuaji wa JFK, alipigwa risasi na Jack Ruby mnamo Novemba 24, kabla ya kushtakiwa. Ruby alikamatwa na kuhukumiwa kwa mauaji ya Oswald.
Ruby alifanikiwa kufuta hukumu yake na hukumu ya kifo lakini akawa mgonjwa na kufa kwa kansa Januari 3, 1967, wakati tarehe ya jaribio lake jipya likiwa limewekwa. Rais Johnson haraka alitoa amri ili kuunda Tume ya Warren-inayoongozwa na Jaji Mkuu Earl Warren-kuchunguza mauaji. Tume hiyo ilihitimisha kwamba Oswald alifanya peke yake kwa kuua Kennedy na kwamba Oswald hakuwa sehemu ya njama yoyote. Matokeo ya uchunguzi huu yanakabiliwa na wengi.

K ILICHOENDELEA BAADA YA MAUAJI
Mnamo Novemba 22, 1963, Kennedy aliuawa huko Dallas, Texas.
Makamu wa Rais Lyndon Johnson alichukua nafasi ya urais baada ya kifo cha JFK.
Lee Harvey Oswald alikamatwa kwa uhalifu wa serikali, lakini aliuawa na kufa na Jack Ruby siku mbili baadaye. FBI na Tume ya Warren wote walimaliza rasmi kwamba Oswald aliyafanya mauaji hayo peke yake. Lakini makundi mbalimbali yalishutumu matokeo ya Ripoti ya Warren na yaliamini kwamba JFK alikuwa mwathirika wa njama. Baada ya kifo cha JFK, Congress ilifanya mapendekezo mengi, ambayo yalijumuisha Sheria ya Haki za Kiraia na Sheria ya Mapato ya mwaka 1964.
Kennedy anaendelea kuwa miongoni mwa marais wakubwa hususani katika sanduku la kura aliyewahi kutawala. Maisha yake binafsi pia yamekuwa ni mtazamo mkubwa wa kupendeza kwa umma. Uuaji huo ulikuwa ni wakati muhimu katika historia ya Marekani kwa sababu ya athari zake kwa taifa, na matokeo ya kisiasa yaliyofuata.
Uchuguzi wa Habari wa Fox wa 2004 uligundua kuwa 66% ya Wamarekani walidhani kulikuwa na njama ya kumwua Rais Kennedy, wakati 74% walidhani kuwa ilikuwa siri ya wachache. Uchunguzi wa kampuni la uchambuzi nchini Marekani wa Gallup Novemba 2013 ulionyesha 61% waliamini kuwa njama, na 30% tu walidhani kuwa Oswald alifanya peke yake. Huwezi kumaliza kumwelezea JFK lakini kwa uchache huo unaweza kupata picha.

IMETAYARISHWA NA: Jabir Johnson
SOURCE: Vyanzo mbalimbali
Sunday, May 26, 2019
Magufuli akutana na Ramaphosa jijini Pretoria
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, John Pombe Magufuli tarehe 26 Mei, 2019 amekutana na kufanya
mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, Ikulu Jijini
Pretoria.
Katika mazungumzo hayo, Rais
Magufuli amempongeza Mhe. Rais Ramaphosa kwa kuapishwa kuwa Rais wa Awamu ya
Tano wa Afrika Kusini na amemhakikishia kuwa Tanzania itadumisha uhusiano na
ushirikiano wa kidugu na kihistoria na nchi hiyo ulioasisiwa na Baba wa Taifa
Hayati Mwl.Julius Kambarage Nyerere na Hayati Nelson Mandela kupitia Chama Cha
Mapinduzi (CCM) na Chama cha ANC (African National Congress).
Rais Magufuli amemshukuru, Mhe
Rais Ramaphosa kwa kumkaribisha kufanya nae mazungumzo siku moja baada ya
kuapishwa kuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Afrika Kusini na amebainisha kuwa
anatarajia uhusiano wa Tanzania na Afrika Kusini utaimarishwa zaidi katika
masuala ya uchumi na kukuza lugha ya Kiswahili.
Kwa upande wake, Rais Ramaphosa
amemshukuru Rais Magufuli kwa kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwake, na
amemhakikishia kuwa Afrika Kusini inatambua mchango mkubwa wa Tanzania katika
ukombozi wa Taifa hilo na kwamba katika kipindi chake cha uongozi wake
atauendeleza na kuuza zaidi uhusiano huo.
Rais Ramaphosa amesema kufuatia
uamuzi wa Afrika Kusini kuanza kufundisha lugha ya Kiswahili, nchi yake
itachukua walimu wa Kiswahili kutoka Tanzania ili watumike kufundisha somo hilo
katika shule za msingi na sekondari.
Aidha, Rais Ramaphosa ameahidi
kufanya Ziara Rasmi ya Kitaifa nchini Tanzania kabla ya Mkutano wa Jumuiya ya
Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) uliopangwa kufanyika mwezi Agosti
2019 nchini Tanzania Na pia atahudhuria mkutano huo.
Kabla ya mazungumzo hayo Rais Magufuli
ambaye ameongozana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Prof. Palamagamba Kabudi amemkabidhi Rais Ramaphosa zawadi ya vitabu vya
kusoma na kufundishia lugha ya Kiswahili kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(UDSM).
SOURCE: Ikulu ya Tanzania
PHOTO BY: CCM Blog
Saturday, May 25, 2019
Mifumo ya urutubishaji shirikishi wa ardhi inayofanywa na TaCRI
Udongo ni maliasili ya kipekee ambayo ndio chanzo cha maisha ya
viumbe na mimea yote iliyopo ulimwenguni, udongo una manufaa mengi
katika maisha ya binadamu, wanyama na viumbe wengine.
Kwa binadamu udongo ndio chanzo cha chakula
cha binadamu kupitia shughuli za kilimo
zinazofanyika kupitia udongo , faida yake kwa binadamu ni
chanzo cha makazi.
Lakini pia kwenye udongo madini yote yanapatikanahuko, hivyo
asilimia kubwa ya shughuli zinategemea udongo, vyanzo vyote vya maji viko
juu udongo, kama vile ziwa, bahari na mito basi maisha ya
binadamu yanategemea udongo.
Udongo ni nini? ‘Udongo’ ni tabaka juu ya ardhi ambalo hufanya kazi kama
chombo cha kukuzia mimea, udongo hujengwa kutokana na shughuli zinazoendelea za
hali ya hewa kulingana na vipengele kadhaa vya mazingira.
Udongo umetengenezwa na nini na unafanya nini? Vitu vya msingi
vinavyotengeneza udongo ni madini, mabaki ya viumbe hai, maji na hewa, udongo
unaofaa kwa ajili ya kukuza mimea mingi huundwa kwa asilimia takribani 45 ya
madini, maji 25 %, hewa 25 %, na mabaki ya viumbe hai 5 %.
Makala yetu kwa leo inaangazia Mifumo ya
urutubishaji shirikishi wa ardhi inayofanywa na taasisi ya Utafiti
wa kahawa Tanzania (TaCRI).
Mtafiti Mkuu wa idara inayohusika na kuongeza tija na ubora wa zao la Kahawa (TaCRI) Suzan Mbwambo, anasema, idara ya udongo imegawanyika katika sehemu kuu tatu, ambayo ni mifumo ya urutubishaji shirikishi wa ardhi (ISFM), mifumo mbalimbali ya makuzi ya kahawa na udhibiti husishi wa visumbufu vya kahawa (IPM).

Anasema maabara ya udongo iliyopo TaCRI, imekuwa ni nyenzo kubwa
katika kuhakikisha kuwa lishe ya Kahawa inaboreshwa na hivyo kutimiza lengo la
kuongeza tija ya kahawa kwa mti.
“TaCRI ilianza kwa kuboresha maabara yake kwa
kununua vifaa ambavyo ni bora na vya kisasa kabisa,
hivyo maabara inauwezo wa kutoa huduma bora na yenye kuaminika ya
uchanganuzi wa uongo, majani na maji kwa wateja mbalimbali ndani na
nje ya tasnia ndogo ya kahawa, lakini kutoa ushauri wa kitaalamu wa matumizi ya
mbolea kulingana na hali halisi ya udongo katika shamba husika,”anasema
Mbwambo.
Mbwambo anafafanua kuwa “Tumefanikiwa pia kufanya tathmini ya rutuba ya
udongo katika maeneo karibu yote yanayolima kahawa hapa nchini hii ikijumuisha
mikoa takribani 16 katika kanda tano zinazolima kahawa hapa nchini
ambapo tayari ripoti zimeshawasilishwa katika wilaya husika, tathmini hii ya
udongo imetuwezesha kubaini maeneo mbalimbali yenye upungufu wa uchachu yaani
(LOW PH),”anasema.
Anafafanua kuwa katika maeneo hayo hata mkulima akitumia mbolea hawezi
kupata mavuno tarajiwa hivyo mkulima atakuwa anatumia gharama kubwa kununua
mbolea na huduma zingine katika shamba lake bila mafanikio yeyote.
Anasema idara hiyo imeanzisha mradi wa majaribio katika maeneo ya wilaya ya
Hai, Rombo, Moshi, Mwanga, Same na Meru kwa upande wa Kahawa aina ya Arabika na
upande wa Robusta ili kuja na mkazo wa jinsi gani ya kurekebisha
uchachu katika maeneo husika na wanatarajia kuanza kufungasha matokeo hayo
kuanzia mwaka ujao.
Mifumo mbalimbali ya makuzi ya kahawa
Mbwambo anasema, Lengo la idara hii ni kuhakikisha kuwa mkulima anaongeza tija kwa mti lakini pia kwa eneo na hivyo basi lishe ni kitu muhimu sana katika kufikia haya lakini pia idadi ya miti inayopandwa kwa eneo ni muhimu sana.

Anasema idara hiyo imeshafanya tafiti katika eneo hilo na
kubaini kuwa idadi ya miti kwa eneo ina tofautiana endapo kama kahawa ni
aina fupi ambayo huhitaji nafasi ndogo, TaCRI imekuwa ikiwashauri wakulima
kuzingatia idadi ya miti katika mashamba yao ili kuweza kupata faida katika
kilimo wanachofanya.
“Yapo majaribio mengi katika eneo hili ambayo kwa sasa yanayendelea
kutunzwa na tunatarajia kuanza kufungasha matokeo ya awali mwaka huu, tumeweza
pia kufungasha teknolojia ya kilimo mseto na migomba , ambapo mkulima anatakiwa
kupanda mistari kitatu ya kahawa yake ndani ya mistari miwili ya
migomba,”anasema Mbwambo.
Anafafanua teknolojia hiyo imepokelewa vizuri sana na wakulima
wengi wa kahawa kwani maeneo yanayolimwa kahawa na migomba pia hustawi vyema,
kilimo mseto cha kahawa na migomba ambacho kinampangilio ambao TaCRI imeufanyia
tathmini unafaida sana kwa mkulima.
Anaongeza kusema kuwa “Kwanza mkulima anauhakika wa kupata chakula kutoka
katika migomba lakini kipato pia, mkulima anauhakika wa kupata
kipato kutoka katika kahawa, msimu ambao sio wa kahawa mkulima atakuwa
anaendelea kupata kipato kutokana na ndizi,”anasema.
Mtafiti huyo anasema, kutokana na mabadiliko ya tabia nchi
kumekuwa na joto sana lakini mvua pia zimekuwa haba, hivyo mkulima ambaye
analima kilimo mseto anaweza kuwa na kilimo endelevu licha ya mabadiliko ya
hali ya hewa, hii ni kwa sababu migomba inatoa kivuli na hivyo basi jua
litakuwa halifiki moja kwa moja katika kahawa na hivyo basi kile kiwango cha
maji kupotea kinapungua kwa kiasi kikubwa.
Anasema ili mti wa kahawa uweze kuwa na tija ya kutosha msimu hadi msimu
na kuendelea kutunzwa vizuri katika maeneo mbalimbali , matokeo ya
awali yanaonyesha tija kubwa imepatikana katika mibuni yenye mashina mengi
ukilinganisha na ile ya shina moja.
Anasema TaCRI inaendelea na utafiti wa kubaini faida mbalimbali
zitokanazo na miche ya kahawa itokanayo na mbegu za
upachikizaji, vikonyo na njia ya chupa, matokeo ya awali yanaonyesha
kuwa mibuni yote inauwezo sawa katika kutoa mavuno na matokeo hayo yanaonyesha
kuwa wadau wa kahawa wanazo njia zaidi ya moja ya kuongeza miche ya kahawa ili
kuhakikisha kuwa tunakidhi haja ya miche ya kahawa kwa wakulima wa kahawa.
Hivyo mtafiti huyo kutoka taasisi ya utafiti wa kahawa nchini
TaCRI Suzan Mbwambo, anawashauri wakulima
kupima afya ya udongo wa mashamba yao kabla ya msimu wa kilimo
kuanza ili kubaini mapungufu yaliyopo katika udongo
na kupata ushauri wa aina gani ya mazo na mbolea zinazoo paswa
kutumika ili kuongeza uzalishaji na tija.
“Ni muhimu sana wakulima wa zao kahawa kufanya zoezi
la kupima udongo kabla ya kutumia mbolea kwani itampa majibu ya
kiasi gani cha mbolea kitumike shambani kwake,”anasema
Mbwambo.
Anaongeza kusema kuwa “Wakulima wengi hawana tabia ya kupima
udongo wa mashamba yao ili kujua tatizo lililopo kabla ya kutumia
mbolea na wengi wamekuwa wakitumia mbolea kwa mazoea bila
kujua tatizo la udongo,”anasema.
Mkuu wa idara ya uboreshaji wa zao la Kahawa kutoka Taasisi ya Utafiti wa
zao la Kahawa nchini TaCRI Dkt Damian Mtenga anasema TaCRI imeweza
kutafiti aina 19 za kahawa aina ya Arabika chotara zenye ukinzani
kwa chulebuni (CBD) na kutu ya majini CLR.
Anasema TaCRI ina aina nne bora za Robusta zenye ukinzani kwa mnyauko
fuzari (CWD), ambazo zinauvumilivu wa magonjwa wa nyauko fuzari, “Aina hizi kwa
kweli zimetafitiwa na zimezalishwa zikizingatia sana ubora na zile
sifa zinazoifanya kahawa iweze kunyweka,”
Dkt Mtenga anasema kahawa iliyofanyiwa utafiti na TaCRI ina sifa za kuzaa
sana na muonjo wake ni mzuri na zina uvumilivu wa magonjwa, na kwamba kahawa
ya Tanzania zaidi ya asilimia 90 inauzwa nje huku
matumizi ya ndani yakiwa ni chini ya asilimia 10.
Dkt Mtenga anasema wakulima wamewezeshwa kuzalisha mbegu mpaya
za kahawa chotara ambapo zinashabikiwa sana , licha ya kwamba TaCRI
haijaweza kuwafikia wakulima wote.
“Kwa upande wa idara yetu kwa sasa katika mkakati wetu wa kuendeleza tafiti
tumekuwa pia tukiangalia masuala ya mabadiliko ya tabia nchi kwa kiwango
kikubwa,”anasema.
Dkt Mtenga anasema kwa sasa TaCRI ipo kwenye mkakati wa kutoa
aina nyingine za kahawa za matazamio ya
aina tatu hadi nne ambazo zina uvumilivu wa ukame.
“Yapo maeneo ambayo tulikuwa tunalima kahawa, lakini kutokana
na mabadiliko ya tabia nchi kahawa sasa hivi haioti tena
katika maeneo hayo na kama ikiota inaota kwa shida, na changamoto
hiyo inatokana na upungufu wa maji, hivyo tunataka katika maeneo
hayo yote tuwe na aina ambazo zinaweza kuendelea kuota,”anasema Dkt
Mtenga.
Anasema ili kuwezesha zao la kahawa kufika
katika uchumi wa kati, TaCRI , imesaidia kuchangia mkakati wa
uzalishaji wa miche ya mbegu chotara za kahawa ambazo zinachangia uzalishaji wa
teknolojia.
STORY & PHOTO BY: Kija Elias