Max Verstappen katika mzunguko wa Yas Marina akipita kwa kasi na kuongoza mazoezi ya siku ya kwanza ya Abu Dhabi Grand Prix 2018 |
Dereva wa magari ya langalanga raia wa Ujerumani Max
Verstappen anaweza kuwa amepoteza hasira zake kali baada ya kuukosa ushindi
kule nchini Brazil baada ya leo katika majaribio kwenye mzunguko wa Yas Marina
kuongoza katika siku ya kwanza ya mbio za Abu Dhabi Dhabi.
Sio kawaida kwa
kampuni la Red Bull kutaka ushindi katika mbio za Abu Dhabi lakini hii leo
imedhihirika katika mazoezi hayo pale alipoongoza kwa dakika 1 na sekunde
38.491 hivyo kuwa mbele ya dereva mwingine wa Red Bull Daniel Ricciardo huku nafasi
ya tatu ikishikwa na Valteri Bottas wa Mercedes.
Lewis Hamilton ameshika nafasi
ya nne na dereva wa timu ya Force India Esteban Ocon waliyegongana na
Verstappen nchini Brazil ameshika nafasi ya tano.
0 Comments:
Post a Comment