Majeneza yaliyobeba miili ya askari yakiagwa katika Kambi ya Kijeshi ya Lugalo jijini Dar es Salaam. |
Miili ya askari watatu wa Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania
(JWTZ) waliofariki dunia wakati wakiwa kwenye operesheni za amani za Umoja wa
Mataifa (UN) imeagwa leo Lugalo jijini Dar es Salaam.
Askari wawili waliuawa
wakiwa kwenye majukumu ya ulinzi wa amani katika Jamhuri ya ya Kidemokrasia ya
Congo (DRC) na mmoja Jamhuri ya Afrika ya Kati. Praiveti Mussa Shija Machibya
na Koplo Mohammed Mussa walipoteza
maisha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati
Koplo Erick Masauri John alipoteza maisha akiwa Jamhuri ya Afrika ya
Kati.
Shughuli za kuagwa askari hao zimefanyika katika viwanja vya hospitali ya
Lugalo na kuhudhuriwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Dkt.
Hussen Mwinyi, vikosi vya ulinzi na usalama na ndugu na jamaa. Miili ya askari
hao iliyowasili jana imesafirishwa katika mikoa ya Mara, Mwanza na Zanzibar
ambako itazikwa.
0 Comments:
Post a Comment