Azkals wakishangilia dhidi ya Singapore katika michuano ya AFF Suzuki mwaka huu |
Michuano ya Soka ya AFF Suzuki Cup imeendelea jana
kukishuhudiwa kikosi cha kocha Sven-Goran Eriksson kikipata ushindi wa bao 1-0
dhidi ya Singapore kwenye mchezo wa kundi B.
Raia huyo wa Sweden anainoa timu
ya taifa ya Ufilipino maarufu Azkals. Kocha huyo wa zamani wa England amechukua
nafasi hiyo hivi karibuni akipokea mikoba ya Scott Cooper na kupata ushindi
wake wa kwanza mjini Bacocold.
Eriksson amesema alama tatu kwenye mchezo huo
ndio jambo la msingi na kuongeza kwamba walicheza vizuri na kutengeneza nafasi
nyingi. Ushindi huo unaifanya Ufilipino kuwa sawa na Thailand, Singapore na
Indonesia.
Kikosi hicho cha Azkals kitakuwa na siku nne kujiandaa dhidi ya
Timor ya Mashariki mchezo utakaochezwa mjini Cheras nchini Malaysia badala ya
mjini Dili huko Timori ya Mashariki kutokana na uwanja kutokuwa tayari kwa
mchezo huo. Leo hakutakuwa na mechi zozote hadi kesho kutwa pale kundi A
litakaposhuka kutafuta alama muhimu katika Kombe hilo.
Sven-Goran Eriksson katika kipindi cha kwanza cha mchezo dhidi ya Singapore |
0 Comments:
Post a Comment