Kisenosato akiangushwa na maegashira Hokutofuji Novemba 13 mwaka huu katika michuano ya Sumo ya Kyushu mjini Fukuoka |
Mashindano
ya Mieleka ya Japan maarufu Kyushu Grand Sumo yameendelea jana Jumanne ikiwa ni
siku yake ya tatu kukishuhudiwa Yokozuna Kisenosato akichemsha dhidi ya
Hokutofuji.
Kupoteza kwa mkali namba moja Maegashira kuliongeza shinikizo kwa
Yokozuna ambaye amepoteza mara tatu mfululizo. Raia wa Mongolia Yokozuna Hakuho na Kakuryu hawakuwapo kutokana na kuwa majeruhi. Hata hivyo matumaini bado yapo
kwa nyota Kisenosato licha ya kuanza vibaya mashindano.
Kisenosato alimpa
mpinzani wake upenyo wa kumsoma hususani upande wa kushoto ambao alionekana
kukosa nguvu kwa upande wa juu kisha kumtoa nje ya mstari.
Hokotufiji
alimshinda Kisenosato baada ya kumbana koo kabla ya kumwangusha kwenye udongo.
Kisenosato alifanya vizuri katika michuano ya Septemba mwaka huu akishinda
10-5. Mashindano hayo yanafanyika mjini Fukuoka nchini Japan.
0 Comments:
Post a Comment