Tuesday, November 27, 2018

Chadema yamjibu Makonda

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda


Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimetetea sababu ya wabunge wake kutoonekana kwenye baadhi ya shughuli za Maendeleo kwa kile walichokidai kuwa wabunge wake hawakupewa mialiko na wengine wakiwa na kesi mbalimbali mahakamani. 

Majibu hayo ya CHADEMA yanakuja ikiwa ni saa chache baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akiwa kwenye uzinduzi wa maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam kusema kuwa wabunge wa upinzani hawaonekani kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo. 

Mkurugenzi wa Itifaki na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema, amesema Makonda anasahau sana kuwa wabunge wetu walifukuzwa kwenye ofisi zao Kinondoni. 

Akiwa kwenye uzinduzi wa maktaba hiyo ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) Paul Makonda amesema amekaririwa akisema anashangaa kuona wabunge upinzani katika mkoa wake wakienda vyuoni kuwarubuni wanafunzi wawapigie kura huku wakishindwa kutokea kwenye shughuli za maendeleo. 

Makonda ambaye mara kadhaa amekaririwa kuwa na kauli tata aliongeza kuwa wapinzani hao kazi yao ni kukosoa tu badala ya kusifia. Hata hivyo Waziri Mkuu wa Zamani na mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema Edward Lowassa alikuwepo katika uzinduzi huo.
Maktaba mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

0 Comments:

Post a Comment