Carlos Ghosn |
Waendesha
mashtaka wa Japan wamemkamata Mwenyekiti wa Kampuni la Magari ya Nissan Carlos
Ghosn kwa kile kinachodaiwa matumizi mabaya ya fedha nchini humo.
Ghosn
amekamatwa baada ya kuhojiwa na waendesha mashtaka wa Japan. Hata hivyo Nissan
imesema itatoa taarifa yake baadaye hii leo. Msemaji wa magari ya Renault na
Renault-Nissan-Mitsubishi hakuweza kuzungumza chochote baada ya tukio hilo.
Mwendesha
Mashtaka wa Umma katika Ofisi ya Wilaya ya Tokyo hakuzungumza lolote kuhusu
kukamatwa kwa mwenyekiti huyo.
Hisa za Renault
zimeanguka jijini Paris kwa asilimia 5.5 ikiwa ni kiwango kibaya kufikiwa kwa
makampuni ya hisa barani Ulaya. Juni mwaka huu Renault ambao ni wanahisa pamoja
na Ghosn walitoa kiasi cha shilingi bilioni 19 kwa ajili ya fidia ya mwaka 2017.
Ghosn mzaliwa
wa Brazil mwenye asili ya Lebanon na mwenye uraia wa Ufaransa ni mwekezaji
mkubwa wa pekee kutoka nje ya Japan. Alianza akiwa na kampuni ya Michelin ya
Ufaransa na baadaye akazama Renault.
Alijunga na
kampuni ya Nissan mwaka 1999 baada ya Renault kununua hisa na ilipofika mwaka
2001 alichukua rasmi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Nissan nafasi aliyodumu nayo
hadi mwaka uliopita.
0 Comments:
Post a Comment