DAR ES SALAAM
Salum Njwete (kushoto) akitolewa mahabusu Machi 22, 2017 |
Kesi inayomkabili
Salum Njwete maarufu Scorpion imeendelea tena leo katika Mahakama ya Wilaya ya
Ilala kwa shahidi wa sita kutoa ushahidi wake.
Shahidi huyu ambaye ni
Meneja wa Baa ya Kimboka ya Buguruni jijini Dar es Salaam Hussein Rashid mwenye
miaka 41 ameiambia mahakama kuwa Scorpion anamfahamu kuwa raia mwema.
Awali mbele ya Hakimu
Mkazi Flora Haule, Mwendesha Mashtaka Nassoro Katuga amedai kuwa shahidi huyo
yupo tayari kuisaidia mahakama.
Shahidi huyo ameiambia
mahakama kuwa anamfahamu Scorpion kama ‘Ticha’
na kwamba ni mlinzi wa amani wa wafanyabiashara wadogo wa Buguruni
aambao huwa wanampatia Shilingi 10,000 kila siku kwa ajili ya kuwalindia bidhaa
zao.
Pia ameiambia mahakama
hiyo kuwa tangu aanze kufanya ulinzi katika maeneo ya wafanyabiashara wadogo
wezi, wakabaji na wale wanaouza vitu vya wizi wametoweka.
Aidha shahidi huyo
amedai kuwa siku ya tukio ‘Scorpion’ alikwenda kwa meneja huyo kwamba kuna
mwizi kapigwa eneo la Shell.
Ilidaiwa mahakamani
hapo kuwa Septemba 6 mwaka jana Scorpion mwenye miaka 34 akiwa Buguruni Shell
alimchoma kwa kisu mlalamikaji Said Mrisho machoni, mabegani na tumboni kisha
kumnyang’anya vitu vya thamani na fedha taslimu.
Kesi hiyo itatajwa tena Aprili 3, mwaka huu.
Kesi hiyo itatajwa tena Aprili 3, mwaka huu.
Salum Njwete baada ya kusikiliza ushahidi wa kesi inayomkabili akirudishwa mahabusu. |
0 Comments:
Post a Comment