NA MWANDISHI WETU
Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam |
Washtakiwa saba wa makosa ya Mtandao kutoka nchi za Pakistan na Sri lanka wamefikishwa mahakama ya
hakimu mkazi Kisutu kujibu mashtaka saba yanayowakabili.
Wamesomewa mashtaka yao
kwa mara ya kwanza ambapo hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na Mahakama
hiyo kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi hiyo hivyo ushahidi utakapokamilia
itasikilizwa mahakama kuu kitengo cha Wahujumu Uchumi.
Washtakiwa hao saba ni pamoja na sita kutoka Pakistan ambao ni Dilshad
Ahmed, Rohail Yaqoob, Khalid Mahmood, Ashfaq Ahmad, Muhamad Aneess na Imtiaz
Ahmad Qammar huku Ramesh Kandasamy akitokea Pakistan.
Mashtaka yao
ni kuingiza vifaa vya mawasiliano bila kibali, kuunganisha vifaa vya mawasiliano
kwenye mitandao ya nchi bila kibali, kuunganisha miundombinu ya mawasiliano nchini
bila kibali, kutumia vifaa vya mawasiliano kuiba fedha kwa mtandao, kuendesha vifaa
vya mawasiliano bila kibali, matumizi mabaya ya mitandao ya mawasiliano na
kufanya kazi bila kibali cha kazi nchini.
Mahakama Kuu ya Tanzania Kitengo cha Wahujumu Uchumi (mahakama ya mafisadi)
ndio yenye uwezo wa kusikiliza kesi hii hivyo watuhumiwa hawakutakiwa kujibu
chochote kwani upelelezi ukikamilika kesi hiyo itasikilizwa mahakama kuu.
Kesi hii imewekwa kwenye kitengo cha
uhujumu uchumi hivyo watuhumiwa wote wamerudishwa rumande mpaka watakapoomba dhamana
Mahakama kuu kitengo cha Uhujumi Uchumi
0 Comments:
Post a Comment