Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) akisoma magazeti muda mfupi kabla ya mahojiano maalum na RFA
|
Hayo yanajiri wakati ambapo jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake likiwa limefunikwa na sakata la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuvamia ofisi za Clouds Media Group akiwa na askari wenye silaha za moto.
Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika mahojiano na Mtangazaji wa RFA Najma Abdallah.
|
Katika mahojiano mubashara na kipindi cha RFA Bonanza cha Redio Free Africa asubuhi ya Machi 20, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho Humprey Polepole amesema anapoonekana mwanachama anakiuka kanuni na utaratibu huwa na subira lakini mwishowe huchukua hatua
“Hakuna aliyewahi kufikiri kama tungechukua uamuzi mkali kabisa wa kuwafukuza uanachama…unapoona kiongozi anakosea ngoja nitumie lugha ya vijana unamlia timing muda utakapokuwa tayari unakula kichwa,” anasema Polepole.
Polepole ameongeza kuwa chama hicho hakiwezi kumwacha kila mtu afanye anachotaka, bali kufanya kwa maslahi ya wananchi ndio kunasisitizwa kila wakati.
Aidha Polepole ametoa wito kwa wanachama kuelekea uchaguzi mkuu wa ndani wa chama hicho kuwa wanapaswa kupiga vita rushwa ili kuendelea kukilinda chama kwani hakiko tayari kuwa na viongozi walioingia kwa rushwa.
Mtangazaji
wa Redio Free Africa, Najma Abdallah
|
Mtangazaji
wa Redio Free Africa, Najma Abdallah akiwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM).
|
0 Comments:
Post a Comment