NA
MWANDISHI WETU
Godbless Lema, Mbunge wa Arusha Mjini |
Awali mahakama hiyo ilimtaka mbunge huyo kuwa na
wadhamini wawili na Shilingi Milioni tatu akini ikafanya marekebisho kwa
kumtaka Lema kusaini bondi ya shilingi milioni 1 ambapo alikidhi vigezo na
kuachiwa huru.
Katika kesi hiyo iliyotolewa maamuzi majira ya saa
7:30 mchana, Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Mjini baada ya kupitia hoja za
mawakili pande zote imemwachia kwa dhamana hiyo kwa masharti ya wadhamini
wawili na kusaini bondi ya shilingi milioni tatu.
Lema amekaa mahabusu kwa takribani miezi minne tangu
alipokamatwa mwezi Novemba mjini Dodoma
na kusafirishwa kupelekwa Arusha kisha kufunguliwa kesi ya uchochezi.
Hali ilivyokuwa baada ya Godbless kuachiwa akitokea gereza la Kisongo nje kidogo ya jiji la Arusha |
0 Comments:
Post a Comment