NA
MWANDISHI WETU
Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) limetoa notisi
ya siku 14 kwa wadaiwa wa Bili za Umeme na baada ya hapo wataendesha zoezi la
ukataji wa umeme nchi nzima huku Wizara na Taasisi za Serikali zikidaiwa
shilingi Bilioni 52,Makampuni Binafsi na
wateja wadogo shilingi Bilioni 94 pamoja na Shirika la Umeme Zanzibar(ZECO)
shilingi Bilioni 127.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo Dk. Tito Mwinuka alisema malimbikizo hayo ya madeni
yamekuwa yakikwamisha jitihada za utekelezaji wa majukumu msingi ndani ya
Shirika hilo ,
na kuongeza limekuwa likipitia wakati mgumu wakati Matengenezo ya miundombinu
pamoja na utekeleza wa miradi mbalimbali.
Dkt. Mwinuka alisema zoezi hilo litakuwa endelevu kwa wadaiwa na
watakoshindwa kulipa madeni na hatua za
kisheria zitachukuliwa kwa wadaiwa hao.
Aidha Dkt. Mwinuka alisema iwapo wadaiwa hao
watalipa malimbikizo ya madeni hayo Shirika litaweza kutatua kwa hatua baadhi
ya changamoto ambazo zinawakabili.
Kwa muda mrefu Shirika la Umeme nchini limekuwa
likilalamikia wateja wake kulimbikiza madeni na wanapoendesha zoezi la
ukusanyaji wa madeni huwa hawafikii malengo.
0 Comments:
Post a Comment