NA MWANDISHI WETU
Shamba la Tumbaku nchini Tanzania |
UZALISHAJI wa zao la Tumbaku kwa wakulima Wilaya ya Chunya (CHUTCU), mkoani
Mbeya umeshuka katika misimu mitatu mfululizo kwa kile kinachodaiwa kuwa ni
kuporomoka kwa bei ya zao hilo
katika soko la dunia.
Taarifa ya Chama Kikuu cha Ushirika wa zao la Tumbaku wilayani Chunya, imebainisha
uzalishaji wa Tumbaku umeshuka kutoka Kilogramu Milioni 13.7 mwaka 2013/2014
mpaka kilogramu Milioni 11.4 zinazotarajiwa kuvunwa katika msimu huu.
Tumbaku likiwa ni miongoni mwa mazao makuu yanayoliingizia Taifa fedha za
kigeni lakini likikosa ushindani mkubwa wa soko huria la wanunuzi ambao kwa
sasa wapo wachache hapa nchini.
Hata hivyo wakulima wa tumbaku wilayani humo wameiomba Serikali kufanya
mazungumzo na China ambayo
inadaiwa kuwa na matumizi makubwa ya tumbaku kwa kununua asilimia 34 ya Tumbaku
inayozalishwa Duniani lakini haijawahi kununua Tumbaku ya Tanzania .
Chama cha Ushirika wa Tumbaku wilayani Chunya, kina wanachama zaidi ya elfu
nane wanaotoka katika vyama 23 vya msingi.
0 Comments:
Post a Comment