BAADHI ya Madaktari wa Idara ya Kinga na Elimu ya Afya kwa Jamii
Muhimbili, wamemlalamikia Kaimu Mkurugenzi, Said Makora kwamba hana uwezo wa
kuongoza kitengo hicho kwa vile hana uwelewa wa fani ya Afya.
Mwenyewe ajibu, kuwa hata Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, hana elimu ya afya lakini anaongoza Maprofesa na
Madaktari.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam, wataalam hao
walisema kuna haja sasa kitengo hicho kuongozwa na watu waliyosomea fani hiyo
ya afya.
Madaktari hao walifikia hatua hiyo baada ya kubaini kuwa mkurugenzi
huyo amekuwa akikiletea aibu kitengo hicho kutokana na kushindwa kijibu masuala
yanayohusu afya pindi anapokutana na wahisani.
"Unajua Kaimu Mkurugenzi wetu hana uwezo wa kutambua masuala ya
afaya kwani yeye ni msomi wa Chuo Kikuu hususan masuala Mawasilano kwa umma
pamoja na yote pia uhusiano wake kikazi na wataalamu siyo wa kuridhisha zaidi
ya manyanyaso,"alisema mmoja wao.
Hata hivyo, walisema kuteuliwa kwa mkurugenzi huyo kumetokana na nguvu
kubwa iliyotumika kutoka kwa baadhi ya vigogo wa walioko katika wizara hiyo,
ambao ndiyo wanaompa kiburi cha kuwanyanyasa madaktari hao.
Makora, alisema kuwa malalamiko hayo hayana msingi bali wanapaswa
kutambua kuwa suala la uongozi na udaktari ni vitu viwili tofauti.
"Ummy mwalimu ana digiree mbili za sheria lakini anawaongoza
wataalamu wa afya kama vile Profesa Bakari wa magonjwa ya binadamu na Dkt.
Mpoki Lisubisya mtalamu wa magonjwa ya usinizi, kwa hiyo mimi ni kiongozi,” alisema
Makora.
Alisema, kutokana na mazingira hayo basi ingekuwa anayestahili kuwa
Waziri angekuwa Prof Bakari, Naibu Waziri Prof Lisubisya huku Ummy akipaswa
kuwa Katibu, hao watu wamezoea kulalamika.
Alisema wanaojua anayefaa kuongoza katika Idara fulani ni serikali na Idara
ya Utumishi na isitoshe yaye ameaminiwa na ofisi ya Katibu Mkuu.
0 Comments:
Post a Comment