Tuesday, April 11, 2017

Wanamtandao waunga mkono juhudi za Dkt. Mbwanji Mbeya

Wanamtandao katika picha ya pamoja wakati wa kupeleka mifuko 11 ya saruji kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Dkt. Mbwanji
Wahenga walisema Uchungu wa Mwana Ajuaye Mzazi, pia wahenga hao walisema Umoja ni Nguvu; hii imejidhihirisha kwa Mkurugenzi wa Hospitali ya Kanda ya Rufaa ya Mbeya Dkt. Godlove Mbwanji kujitolea kujenga wodi moja kwa ajili ya watoto.
Chanzo chetu kilitujuza kuwa kilichomsukuma Dkt. Mbwanji ni baada ya kuona ongezeko la wagonjwa hususani watoto ni kubwa ndipo alipoamua kujenga wodi maalum.
Hata hivyo kundi moja la Watu wanaojihusisha na mitandao ya kijamii mkoani humo lilipoona juhudi za mtalaamu huyo likajichangisha mifuko 11 ya saruji ili kuunga mkono juhudi hizo.
“Ujenzi bado unaendelea wa wodi hiyo. Tunaamini ikishamalizika itakuwa msaada mkubwa sana kwa watoto wanaotibiwa katika hospitali yetu,” kilisema chanzo hicho
Hadi sasa bado blog hii haijapata ujenzi huo utagharimu kiasi gani kwa mwenye maelezo ya kina unaweza kutuma katika namba ifuatayo. 
+255-(0)-768 096 793




0 Comments:

Post a Comment