Papa Francis akisalimia na Abdel Fatah al-Sisi baada ya kuwasili |
Papa Francis akisalimiana na Sheikh Ahmed al-Tayeb |
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis, amewasili katika
Chuo Kikuu cha Al-Azhar nchini Misri, kinachotambuliwa kuwa kituo kikuu cha
elimu kwa Waislamu wa madhehebu ya Sunni, kukutana na Imam Mkuu wa Misri Sheikh
Ahmed al-Tayeb.
Awali Papa Fancis mwenye umri wa miaka 80, alikutana na Rais Abdel
Fattah al-Sisi aliyemkaribisha kwa bendi ya kijeshi pamoja na mapadri
waliojipanga kumsalimia Papa huyo.
Papa amesema ingawa ni safari ya siku mbili lakini ina umuhimu sana kwa
kuwa ni safari ya umoja na udugu.
Leo la safari hiyo ni kutaka kuimarisha mahusiano na viongozi wa dini
ya Kiislam katika wakati ambapo jamii ya kale ya Kikiristo nchini Misri
inakabiliwa na shinikizo kubwa kutoka kwa wanamgambo wa kundi linalojiita Dola
la Kiislam (IS), wanaotishia kuitokomeza jamii hiyo.
Papa Francis akipunga mkono. |
0 Comments:
Post a Comment