MAIDUGURI, NIGERIA
Chibok Girls |
Leo imetimia miaka mitatu kamili tangu kundi la kigaidi la Boko Haram
lilipowateka wasichana zaidi ya 270 kutoka shuleni kwao katika kijiji cha
Chibok kaskazinimashariki mwa Nigeria.
Katika idadi hiyo, wasichana kadhaa walifanikiwa kutoroka au kuachiwa
huru, lakini wengine 195 bado hawajapatikana. Msemaji wa rais wa Nigeria Garba
Shehu amesema serikali inajadiliana kwa msaada wa mataifa na mashirika ya
kigeni ili kufanikisha kuachiwa kwa wasichana wanaoendelea kushikiliwa na kundi
la Boko Haram.
Shehu amesema wasichana 21 walioachiwa kwa msaada wa shirika la misaada
la Msalaba Mwekundu ICRC na maafisa wa serikali ya Uswisi, na kuongeza kuwa
ICRC na serikali ya Uswisi wanaendelea kuunga mkono majadiliano hayo.
Boko Haram iliwateka wanafunzi 276 kutoka shule ya sekondari ya
serikali mjini Chibok Aprili 14, 2014.
0 Comments:
Post a Comment