Mfalme Salman aliwahi kuwa Naibu Gavana wa Riyadh na baadaye Gavana wa Riyadh kwa miaka 48 tangu mwaka 1963 hadi mwaka 2011.
Mfalme Salman aliwahi kuteuliwa kuwa Waziri wa Ulinzi wa taifa hilo la Kiislamu. Mnamo mwaka 2012 alitangazwa kuwa mrithi wa ufalme huo baada ya kifo cha kaka yake Nayef bin Abdulaziz.
Salman alikuja kuwa Mfalme mpya wa Saudia Januari 23, 2015 baada ya kifo cha kaka yake Mfame Abdullah. Tangu mwaka 2019 Mfalme Salman ndiye mtoto pekee wa Ibn Saud aliye hai.
Katika masuala ya kusimamia taifa hilo Mfalme Salman aliingia kati mzozo wa kivita wa Yemen na kutangaza kumtambua Abdrabbuh Mansur Hadi mwenye asili ya Saudia Arabia kuwa kiongozi mkuu wa Yemen.
Pia Mfalme Salman tangu aliposhika madaraka hayo anasimamia maono ya ifikipo 2030 taifa hilo lisiwe tegemezi katika biashara yake ya mafuta kuboresha sekta ya afya, elimu, miundombinu na utalii.
Mnamo mwaka 2017 Mfalme Salman atakumbukwa kwa kuwaruhusu wanawake kuendesha magari kwani hapo awali kwa miaka mingi wanawake hawakuwa na uhuru wa kuendesha vyombo vya usafiri.
Pia mwaka huo huo Mfalme Salman aliingia katika mkanganyiko kufuatia mauaji ya mwanahabari Jamal Kashoggi ambayo yanadaiwa kufanywa na familia hiyo ya Kifalme ya Saudi Arabia.
Pia Mfalme Salman aliingia katika sintofahamu nyingine baada ya kuwakamata wanafamilia wa Kifalme, mawaziri wake, wafanyabiashara ikiwa ni majuma machache baada ya kuundwa kwa tume ya Mapambano dhidi ya Rushwa iliyoongozwa na Crown Prince Mohammad bin Salman maarufu MbS.
Mfalme Salman anatajwa kuwa ni mtoto wa 25 wa Abdulaziz ibn Abdul Rahman ibn Faisal ibn Turki ibn Abdullah ibn Muhammad Al Saud kwa watu wa magharibi hufupisha Ibn Saud, ambaye ndiye mwasisi wa taifa hilo la Kiislamu.
Salman alikulia katika jumba la kifalme la Murraba ambalo kwa sasa ni makumbusho katika viunga vya Riyadh. Salman alisoma elimu ya awali katika shule ya Watoto wa Kifame ya Prince’s iliyopo katika mji mkuu wa Saudia Arabia Riyadh.
Ibn Saud alianzisha shule hiyo kwa ajili ya watoto wake ili waweze kupata elimu. Salman alisoma elimu ya dini na Sayansi ya Kisasa.
Alipoingia madarakani alifanya mabadiliko kadhaa ya utawala wake ambapo Khalid bin Ali bin Abdullah al-Humaidan alimfanya kuwa mkuu wa usalama wa taifa.
Prince Bandar bin Sultan aliondolewa katika idara hiyo ya ulinzi. Baadaye katika utawala wake aliingia katika kashfa ya nyaraka za siri kuvuja kwa kile kilichofahamika kama Panama Papers ambapo ndani yake kulikuwa na makampuni makubwa mawili kutoka Britisha Virgin Islands pia Crown Prince Muhammad bin Nayef alitajwa katika kashfa hiyo. Salman ameoa mara tatu katika maisha yake.
Hadi mwaka 2017 alikuwa na watoto 13 mkewe wa kwanza Sultana bint Turki Al Sudairi alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 71 mapema Julai 2011, baadaye alimuoa Sarah binti Faisal Al Subai’ai ambaye waliachana na kwa sasa anaye Fahda bint Falah Al Hathleen.
Mtoto wake wa kwanza Fahd bin Salman alifariki dunia akiwa na miaka 47mnamo Julai 2001 kwa ugonjwa wa moyo. Pia mtoto wake wa tatu wa kiume Ahmad naye alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 43 mnamo Julai 2002 kwa ugonjwa wa moyo.
Salman ndiye mwarabu wa kwanza na muislamu wa kwanza kusafiri katika anga za juu akifanya hivyo kwa kutumia kifaa STS-51-G mnamo Juni 1985.