Andre Bocelli |
Mwimbaji wa muziki nchini Marekani Celine Dion aliwahi kusema " Kama Mungu angekuwa na sauti ya uimbaji, angeimba kama Andrea Borcelli. " Pia prodyuza David Foster aliwahi kusema kuhusu Borcelli kuwa ni mwimbaji mwenye sauti nzuri kuliko wote duniani. Hadi sasa amerekodi albamu 15 za muziki na kuuza zaidi ya kopi zaidi ya milioni 80.
Mwaka 1998 Bocelli alitajwa katika Jarida la People kuwa miongoni mwa watu 50 bora wanaovutia duniani. Mwaka 1999 alishiriki katika tuzo za Grammy. Katika medani hiyo ya muziki akiwa na miaka 33 alikuwa bado anapiga kinanda (piano) katika maeneo ya baa. Bocelli alizaliwa kwa wazazi Alessandro na Edi;
Wakati akiwa tumboni mwa mama yake, ilielezwa kuwa daktari alimtaka mamaye kutoa mimba hiyo kwani ingemletea matatizo lakini alipuuzia hatimaye alimzaa Andrea. Katika makuzi yake akiwa na familia yake alikuwa akiuza vifaa vya shambani na kutengeneza mvinyo katika kijiji kidogo cha La Sterza, Tuscany takribani kilometa 40 kusini mwa mji wa Pisa. Baba yake alifariki mwaka 2000.
0 Comments:
Post a Comment