Maadhimisho hayo yametanguliwa na Uelimishaji ambao unafanywa na WWF kwa kushirikiana na idara mbalimbali za serikali kwa kutumia njia tofauti ikiwemo maonesho ya shughuli za uhifadhi wa maliasili/wanyapori.
Afisa Miradi wa WWF uwanda wa Ruvuma Richard Katondo alisema dhima hasa ya maadhimisho ni umuhimu wa kila kijiji kuwa na mpango bora wa matumizi ya ardhi ambao una ainisha maeneo ya kilimo, ufugaji, uhifadhi pamoja na mipaka ya kijiji huku ukishirikisha wananchi katika kila hatua ili kuondoa migogoro.
0 Comments:
Post a Comment