Mfamasia akimhudumia mteja wake |
Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Wafamasia (FIP) Dkt. Carmen Peña katika taarifa yake iliyotolewa kupitia wavuti ya hilo katika kuadhimisha siku ya Mfamasia Duniani imesema Wafamasia wamekuwa wakiongezeka mwaka na kwamba kuanzia 2016 na ifikapo mwaka 2030 inatarajiwa kufikia asilimia 40.
Aidha taarifa ya shirikisho hilo imesema Septemba 25 ambayo ni leo ni maalum ya Wafamasia wote ulimwenguni kuitumia kwa kutoa elimu na ushauri kuhusu utoaji wa madawa kwa madhumuni ya kuboresha afya za watu.
Hata hivyo ripoti iliyotolewa mwanzoni mwa mwezi huu jijini Glasgow, nchini Scotland katika Kongamano la 78 la Dunia katika Ufamasia na Sayansi ya Ufamasia imeweka bayana kuwa nchi zenye uchumi mdogo zimekuwa zikipambana na ukuaji mdogo wa Wafamasia.
Zaidi ya Wafamasia milioni nne ulimwenguni kote wanaadhimisha siku hii ambayo ilianzishwa mwaka 2009 jijini Istanbul nchini Uturuki na Shirikisho la Kimataifa la Wafamasia (FIP).
0 Comments:
Post a Comment