Neymar Jr. akimliki mpira mbele ya Mohamed Salah katika mchezo wa Kundi C wa ligi ya mabaingwa barani Ulaya usiku wa Septemba 18, 2018 Anfield |
Roberto Firmino akiingia kuchukua nafasi ya Daniel Sturridge |
Pongezi kwa mshambuliaji wa Brazil akitokea benchi Roberto Firmino alipoingia kuchukua nafasi ya Daniel Sturridge na kutupia bao la ushindi katika kikosi cha Jurgen Klopp. Sturridge alianza kufungua ukurasa kwa bao la kichwa katika dakika ya 30 kabla ya James Milner hajaipa uongozi Liverpool kwa mkwaju wa penati baada ya Georginio Wijnaldum kuangushwa katika eneo la hatari.
Mfaransa Thomas Meunier aliirudisha PSG na baadaye Kylian Mbappe aliisawazishia PSG katika dakika ya 82 kabla ya Firmino kuharibu mahesabu ya matajiri hao wa Paris katika dakika ya 90. Neymar Jr na Edinson Cavani hawakuwa na ujanja mbele ya vijana wa Klopp huku Klopp mwenyewe akikutana na Thomas Tuchel waliyewahi kufanya naye kazi walipokuwa Borussia Dortmund na kuipa mafanikio makubwa katika historia ya klabu hiyo ya Bundesliga.
0 Comments:
Post a Comment