Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe |
Tukio hilo linatarajiwa kufanyika asubuhi ya leo huku wadau mbalimbali wakialikwa zikiwemo sekta na taasisi mbalimbali za umma, sekta binafsi, taasisi na asasi za kimataifa, balozi mbalimbali,vyombo vya habari, taasisi za dini na taasisi za kitaaluma.
Taarifa ya chama hicho imebainisha katika tukio hilo vyombo na taasisi mbalimbali za Serikali kama Mkuu wa Jeshi la Polisi, Gavana wa Benki Kuu, Msajili wa Vyama vya siasa na taasisi nyingine zimealikwa.
Katika uzinduzi huo Chadema itaweka hadharani misimamo ya kisera kwenye maeneo mbalimbali ya uchumi, afya, elimu na sayansi, miundombinu, maji, mfumo wa Utawala, Katiba na haki za binadamu, Masuala ya Muungano, Mambo ya Nje na Uhamiaji, Siasa za ndani, Usimamizi wa Ardhi na Kilimo pamoja na Mazingira.
0 Comments:
Post a Comment