Wasifu wa Suleiman Nyambui
Nyambui alizaliwa Februari 23, 1953 Majita, Musoma mkoani Mara. Aliacha shule na kuanza kazi ya uvuvi katika Ziwa Victoria wilayani Ukerewe mkoani Mwanza. Baadaye alijiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ambako alijifunza mambo mbalimbali ya kulisaidia taifa.
Pia aliwahi kuwa mwalimu katika Shule ya Bukumbi iliyopo kilometa 32 kutoka jijini Mwanza kabla ya kukwea pipa kwenda nchini Marekani. Akiwa nchini Marekani alisoma katika Chuo Kikuu cha Texas El Paiso (UTEP) shahada ya kwanza na uzamivu. Baada ya kumaliza mkataba wake na Bahrain alirudi Tanzania na kushika wadhifa wa Katibu Mkuu wa RT hadi alipoachia Juni mwaka huu.
Muda mzuri aliowahi kukimbia
Mita 1500: dakika 3:35.8
Maili: dakika 3:51.94
Maili 2: dakika 8:17.9
Mita 5000: dakika 13:12.29
Mita 10,000: dakika 27:51.73
Marathon: saa 2:09:52
SULEIMAN NYAMBUI
0 Comments:
Post a Comment