Mratibu wa mradi wa Vicoba Shirikishi Hellen Mushi akihamasiisha wananchi katika kata ya Njiapanda kujiunga na mradi huo unaojihusisha na watu wenye ulemavu na wasio na ulemavu |
Hayo yalisemwa na Mratibu
wa mradi wa Vicoba shirikishi kupitia shirika la TUSONGE Hellen Mushi wakati
alipokuwa akizungumza kwenye kongamano lililofanyika katika ofisi za kata Njia
Panda mjini Moshi.
Mushi alisema, “Watoto
hao tunawafikia kupitia wazazi wao ambao ni wanachama wa vikundi vya Vicoba
Shirikishi ambavyo viko chini shirika letu la TUSONGE.”
Aidha mratibu huyo
alisema changamoto mbalimbali katika jamii ndizo zilizosababisha kuingia kwa kina
katika kufuatilia baada ya wazazi wao ambao ni wanachama wa shirika hilo.
Deogratius Chami miongoni mwa watu wenye ulemavu akielimisha kuhusu haki za watu wenye ulemavu katika Kata ya Njiapanda mjini Moshi |
“Mila na desturi
zinazowazunguka ndizo chanzo kikubwa kinachosababisha wimbi kubwa la watoto
kufichwa ndani, lakini kupitia mradi wetu huu tumewafikia hao kwani nao ni
binadamu ambao wana mahitaji sawa na wengine,” alisema Mushi.
Alisema asilimia 40 ya
watoto hao wameshafikisha umri wa kwenda
shule , lakini hawajaweza kupelekwa
shule na wazazi wao kwa kukosa huduma za afya na utengamao.
Mushi aliongeza kuwa
kupitia mradi huo wamefanikiwa kuwaunganisha watoto hao na CCBRT ambao wamekuwa
bega kwa bega katika kufuatilia watu wenye ulemavu hao.
Mwenyekiti wa Umoja wa Watu wenye Ulemavu Njiapanda Thadei Mbuya akizungumza na hadhira ya watu waliohudhuria kongamano la watu wenye ulemavu. |
Nae Afisa wa CCBRT anayesimamia kata ya Njiapanda
Gladness Mushi alitoa hamasa kwa wazazi na viongozi wa serikali kuwaleta watoto
wenye ulemavu kliniki ili wapate huduma ya utengamao.
Mradi wa Vicoba
shirikishi uliopo Kata ya Njia Panda Himo wilaya ya Moshi, unafadhiliwa na African
Initiatives na National Community Lottery Fund kutoka nchini Uingereza, yakiwa
na dhamira ya kuwaunganisha watu wenye ulemavu ili wajikwamue kiuchumi na
kuachana na utegemezi.
Baadhi ya watu waliohudhuria kongamano la Mradi wa Vicoba Shirikishi kata ya Njiapanda Aprili 26, 2019. |
STORY BY: Kija Elias
EDITED BY: Jabir Johnson
PHOTO BY: TUSONGE CDO
0 Comments:
Post a Comment