Wakati kocha wa klabu ya Manchester United
Ole Gunnar Solskjaer akijitahidi kuigeuzia kibao Paris Saint Germain katika
hatua ya 16 na kutinga robo fainali na kusonga mbele katika Ligi ya Mabingwa
barani Ulayani, swali limesalia katika hatua hiyo kama ataweza kutoboa baada ya
kuzabuliwa kwa bao 1-0 na Barcelona ambao walianzia ugenini Old Trafford.
Bao
pekee la kujifunga la Luke Shaw liliwapa miamba hiyo nafasi ya kuwa kwenye
nafasi nzuri ya kutonga hatua ya nusu fainali.
Je, mashetani wekundu wanaweza
kugeuza kibao tena watakapotua Camp Nou kuwakabili wenyeji wa dimba hilo gumu?
Maroune Fellaini ndiye mchezaji wa mwisho wa klabu hiyo kufunga bao katika ligi
ya mabingwa katika dimba la Old Trafford, alifanya hivyo Novemba 27, 2018.
Manchester
inaendelea kupambana katika ligi ya mabingwa kwa msimu wa nne sasa.
Martial angeweza kuifungia Manchester United lakini Gerard Pique alifanikiwa kuondoa hatari ndani ya boksi. |
Lionel Messi na Luis Suarez wakishangilia baada ya kusababisha bao pekee katika mchezo wao dhidi ya Manchester United |
Novemba 27, 2018 Maroune Fellaini alifunga bao katika uwanja wa Old Trafford. |
0 Comments:
Post a Comment