Saturday, April 6, 2019

Wanawake 10 wakamatwa na mirungi Kilimanjaro

MOSHI, KILIMANJARO 
Wanawake wanane wamekamatwa na Jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro kwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya aina ya mirungi. 
Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi ACP Hamisi Issah
Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro ACP Hamis Issah alisema watuhumiwa hao walikamatwa kwa nyakati wilayani Moshi na Hai Aprili 3 mwaka huu. 
ACP Issah aliongeza kuwa kilo 36 za dawa za kulevya walizikamata kwa wanawake hao. Waliokamatwa ni Lilian Kombe (34), Nora Molel (45), Ivon Kitomary (18), Hilaria Samson (55), Pendo Nko (25), Mwanahamis Salehe (40), Nimwindael Mvungi (37) na Husna Juma (25). 
Jeshi la Polisi lilisema watuhumiwa hao wamekamatwa katika maeneo tofauti ya Matindigani, Maili Sita, Kizuizi cha Wasomali-Hai, Njiapanda-Himo na Himo Stendi.

Aidha ACP Issah alisema wanawake hao walikamatwa wakiwa katika harakati za kusafirisha kwa ajili ya wateja wao. 
ACP Issah katika kituo cha Polisi cha Kati mjini Moshi na watuhumiwa wa dawa za kulevya aina ya mirungi
Hata hivyo Kamishna huyo alisema biashara ya mirungi imekuwa ikiwatesa mno katika mkoa huo lakini biashara kubwa inafanyika zaidi mkoani Arusha. 

“Imekuwa ikisafirishwa kutoka nchi jirani na kwenda Arusha ambako ndiko soko kubwa liliko, imekuwa ikitutesa sana lakini juhudi za kupambana zinaendelea kutoka kwa vijana wetu shupavu,” alisema ACP Issah.

Katika mahojiano yaliyofanyika katika makao makuu ya jeshi hilo mkoani Kilimanjaro wanawake hao walisema changamoto ya maisha inawafanya kutafuta mbinu namna ya kuzilisha familia zao na ndio sababu ya kujiingiza katika biashara hiyo haramu.
Hata hivyo ACP Issah aliwataka watanzania kutambua kuwa ugumu wa maisha isiwe gia ya kuwafanya wavunje sheria na kwamba watuhumiwa hao watapandishwa kizimbani kujibu mashtaka yanayowakabili. 
Baadhi ya mirungi iliyokamatwa na Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro. Polisi nchini humo ilisema inapata wakati mgumu kuzuia biashara hiyo ambayo inatokea nchini Kenya.
Mbali na kuwamata wanawake ACP Issah aliongeza kuwa katika maeneo ya Pasua mjini Moshi mtuhumiwa ambaye hadi sasa hajafahamika aliwakimbia Polisi na kuiacha pikipiki yake yenye namba za usajili MC. 375 AFN aina ya Wanhoo. 
Baada ya kuipekea pikipiki hiyo walikuta gramu 180 za mirungi. Pia ACP Issah alisema wamewakamatwa watu ambao wamekuwa wakiwasaidia kuwapa taarifa wasafirishaji, wauzaji wa mirungi kuhusu uwepo wa askari polisi katika maeneo mbalimbali. 
“Richard Mwanamosha (34), Steven Massawe (44), Amina Msangi, Abdallah Shafii (27) na Tumaini Massawe (16) tumewakamata kwa kujihusisha na biashara ya mirungi, wamekuwa wakiwapa wenzao taarifa za uwepo wa askari polisi katika maeneo mbalimbali, nao tutawapandisha kizimbani,” alisema ACP Issah.
Story by: Jabir Johnson
Photography: Kija Elias

0 Comments:

Post a Comment