Thursday, April 18, 2019

Simba SC yapanda viwango CAF, Yanga hoi


Klabu ya Simba ya Tanzania imepanda kwa alama 465 katika viwango vya ubora wa vilabu vya soka barani Afrika kama inavyotolewa na FootballDatabase. 
Viwango hivyo vilivyotolewa Aprili 14 mwaka huu vinaonyesha klabu hiyo imeshika nafasi ya 257 kati ya klabu 501 zinazotambulika barani Afrika katika orodha hiyo. 

Kwa nafasi hiyo inakuwa klabu ya kwanza nchini Tanzania ikiwapita mahasimu wao Young Africans ambayo imeshika nafasi ya 359 ikishuka kwa alama tisa. Azam FC imeshika nafasi ya 378 ikiwa imepanda alama 71. 

Katika orodha hiyo Difaa El Jadida ya Morocco aliyopo mchezaji wa Tanzania Simon Msuva inashika nafasi ya 43 ikiwa imeshuka kwa alama 67 huku JS Saoura ya Algeria anayochezea Mtanzania Thomas Ulimwengu imekalia nafasi ya 45 ikipanda kwa alama 114. 

Nafasi ya 77 imeshikwa na ENPPI aliyopo Mtanzania Shiza Kichuya ikishuka kwa alama 138. Petrojet ya Misri aliyopo Mtanzania Himd Mao Mkami inashika nafasi ya 163 ikishuka kwa alama 348.

12 Bora za Afrika ngazi ya Klabu 
Esperance de Tunis (Tunisia) 
Al Ahly (Misri)
TP Mazembe (DR Congo)
 Al Merreikh (Sudan)
 Etoile du Sahel (Tunisia)
AS Vita (DR Congo)
 Wydad Casablanca (Morocco)
 Al Hilal Omdurman (Sudan)
 CS Sfaxien (Tunisia)
               El Zamalek (Misri)
       Mamelodi Sundown ( Afrika Kusini)
           1 de Agosto (Angola)


0 Comments:

Post a Comment