Afisa Elimu
Takwimu wa Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro Herman Msasa ametoa ahadi ya
kuwasomesha wanafunzi watakaopata daraja la kwanza katika matokeo ya kidato cha
nne.
Akizungumza
katika ziara ya kutembelea na kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa katika
Shule za Sekondari za Matadi, Karansi na Sikirari wilayani humo Msasa alisema
serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeweka kipaumbele katika suala la
elimu kwa kuendelea kutoa elimu bure kwa wanafunzi hivyo ni juu ya wanafunzi
hao kuitumia fursa hiyo vizuri kwa kujipatia ufaulu wa daraja la juu.
Msasa
alisema kwa jamii ya wafugaji wilayani humo imeitikia wito wa serikali kwa
kuwapeleka watoto wao katika shule za sekondari
hivyo kupunguza wimbi la kutokuwa na makazi rasmi ya kuishi kutokana na
tabia ya kuhamahama.
“Ahadi yangu
inabaki palepale, siwezi kushindwa kuwasomesha watoto kidato cha tano na cha
sita endapo mtafaulu na kupata division one,” alisema Msasa.
Katika ziara
hiyo Msasa aliwataka wanafunzi hao kuachana na tamaa zisizo za lazima na
kujitahidi kwa udi na uvumba kusoma kwa bidii kwani kufaulu kwao ndio maendeleo
ya nchi kwa ujumla.
Matadi Secondary School, Siha Kilimanjaro |
Afisa Elimu Takwimu wilaya ya Siha Herman Msasa akizungumza na wanafunzi wa sekondari ya Karansi katika ziara shuleni hapo hivi karibuni. |
Mkuu wa Wilaya ya Siha Onesmo Buswelu akionyesha mfano wa ujenzi katika sekondari ya Karansi katika ziara ya kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa na mabweni. |
Katika ujenzi wa vyumba vya madarasa serikali imepeleka kiasi cha shilingi milioni 135 katika shule ya Sikirari na katika shule ya sekondari Karansi imepeleka shilingi milioni 115 na shilingi milioni 25 katika shule ya sekondari ya Matadi kwa ajili ya kumaliza vyumba vya madarasa.
Kwa upande
wake Mkuu wa Wilaya hiyo Onesmo Buswelu alisisitiza kuwa ujenzi wa madarasa utapunguza msongamano, na
kurahisisha suala la ufundishaji wa wanafunzi kwa walimu.
Mkuu wa Wilaya ya Siha Onesmo Buswelu akiwa katika sekondari ya Sikirari katika ziara ya kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa. |
Mwishoni mwa mwaka huu kidato cha nne watakuwa
wakifanya mitihani yao ya kuhitimu elimu yao ya sekondari.
0 Comments:
Post a Comment