Serikali imeanza kutekeleza mradi mkubwa wa maji unaojulikana
kama “Arusha Sustainable Urban Water and Sanitation Delivery Project” ambao
utaboresha huduma ya Majisafi na Usafi wa Mazingira katika Jiji la Arusha na
baadhi ya maeneo ya wilaya za Arumeru na
Hai.
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha Mhandisi Ruth Koya, wakati alipokuwa akitoa taarifa yake mbele ya kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Hai, kwenye ziara ya kutembelea mradi wa uchimbaji wa visima virefu 18 vya maji vinavyochimbwa katika wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, kwa ufadhili wa Benki ya Maendeleo Afrika (AFDB) na Serikali ya Tanzania.
Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya akionja maji ya kisima kilichochimbwa na Mradi wa Arusha Sustainable Urban Water and Sanitation Delivery kwa udhamini wa Benki ya AfDB |
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha Mhandisi Ruth Koya, wakati alipokuwa akitoa taarifa yake mbele ya kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Hai, kwenye ziara ya kutembelea mradi wa uchimbaji wa visima virefu 18 vya maji vinavyochimbwa katika wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, kwa ufadhili wa Benki ya Maendeleo Afrika (AFDB) na Serikali ya Tanzania.
Mhandisi Koya alisema mradi huo ulianza kutekelezwa Julai
2018 na Mradi huo utarajiwa kukamilika Julai 2020, ambapo hadi kukamilika kwake
utagharimu kiasi cha fedha Bilioni 476 za Kitanzania.
Mhandisi Koya alisema mradi huyo umelenga kuhakikisha Jiji
la Arusha linaondokana na changamoto ya maji inayoikabili kwa sasa na kwamba
kukamilika kwa mradi huo kutaweza kuwapa wananchi huduma hiyo muhimu.
“Mradi huu utagharimu jumla ya dola za Marekani milioni 233,915,581,11 sawa na shilingi za Tanzania
bilioni 476, ambapo katika fedha
hizo kiasi cha dola za Marekani milioni 210,962, 581.00 ni mkopo wenye masharti
nafuu kutoka Benki ya Maendeleo ya
Afrika AFDB na kiasi cha dola za Marekani milioni 22,953,000.00 ni
mchango wa serikali ya Tanzania.
Alisema kutokana na
kasi ya ukuaji wa Jiji la Arusha,
utoaji wa huduma za Majisafi na uondoaji
wa majitaka umekuwa hautoshelezi mahitaji ya wakazi wote, hivyo kukamilika kwa mradi huo utaweza kutatua
changamoto iliyopo katika Jiji hilo.
Mhandisi Koya alisema
kazi kubwa zilizopangwa kutekekelezwa kwenye mradi huo zilikuwa ni pamoja
na utafutaji wa vyanzo vya maji,
uchimbaji wa visima virefu, ujenzi wa matenki, ulazaji wa mtandao wa Majisafi
na Maji taka.
Kazi nyingine ni
ujenzi wa mitambo ya kutibu maji, ujenzi wa mabwawa mapya ya kusafisha
majitaka, ununuzi wa vitendea kazi,
ujenzi wa ofisi kuu ya Mamlaka na ofisi za Kanda.
“Lengo la mradi huu ni kuboresha hali ya upatikanaji wa
Majisafi na kuboresha huduma ya uondoaji
wa Majitaka katika Jiji la Arusha
ili kuboresha afya na hali ya maisha ya wakazi wa Jiji hilo kwa ujumla
wake.”
Alifafanua kuwa Mradi huo unatarajiwa kukamilika Mwaka 2020
na baada ya kukamilika huduma za
Majisafi na uondoaji wa majitaka zitakuwa zimeboreshwa katika Jiji hilo.
Akizungumza mara baada ya ziara kukagua mradi huo Mkuu wa
wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya, alisema serikali imekuwa ikichukua kwa haraka
changamoto ambazo zimekuwa zikiwakabili
wananchi kwa ujumla.
“Upatikanaji wa maji kwa wilaya ya Hai upo kwa wango cha juu na
hilo limethibitishwa na watafiti
waliofanya utafiti katika wilaya ya Hai
na kuona kuwa kuna maji meng,”alisema DC
Sabaya.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa
halmashauri ya Wilaya ya Hai Yohana
Sintoo, alisema ukanda wa tambarare ndio ambao mara nyingi umekuwa
ukikumbwa na changamoto ya upungufu wa maji
hususani katika kipindi cha kiangazi, kutokana na vijiji vya tanbarare
kutegemea vyanzo vya maji vilivyopo maeneo ya milimani.
“Nia ya serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk John
Magufuli ni kuhakikisha wananchi wake wanapata Maji safi na salama hivyo,
kukamilika kwa mradi huu, kutawaondolea changamoto wananchi wa vijiji vya
Chekimaji na Ngosero ambao wananufaika na
mradi huo kwa kujengewa visima hivyo vya maji vinavyo chimbwa katika
maeneo yao,”alisema Sintoo.
STORY by: Kija Elias
PHOTOS by: Kija Elias
EDITED by: Jabir Johnson
0 Comments:
Post a Comment