|
Philemon Ndesamburo, enzi za uhai wake |
“Salaam zangu za rambirambi Kwa dada yangu mpenzi
Lucy Owenya Kwa kupotelewa na baba mzazi Mzee Philemon Kiwelu Ndesamburo. Ni
msiba mkubwa Kwa watu wa Kilimanjaro na hasa Moshi Mjini ambapo Mzee Ndesa Pesa
alikuwa mwakilishi wake Bungeni kuanzia Mwaka 2000 mpaka Mwaka 2015.
Kilimanjaro imepoteza mtu ambaye aliweka maslahi ya mkoa wake mbele kuliko kitu
kingine chochote. Ni msiba mkubwa Kwa wanachama wa CHADEMA ambacho alikuwa
Mwenyekiti wake Wa Mkoa tangu Chama kimeanzishwa mpaka mauti yalipomkuta.
Huwezi kutaja maendeleo ya CHADEMA kwa nchi yetu bila ya kutaja jina la Mzee
Ndesamburo. Nimepata bahati ya kufanya naye kazi Kwa karibu, naweza kutamka
bila wasiwasi kwamba ni mmoja wa watu waliokipenda Chama chake Kwa dhati
Kabisa. Ni msiba mkubwa Kwa Watanzania. Mzee Ndesamburo alitumia uwezo wake Wa
kifedha na kiakili kuimarisha mfumo wa Vyama vingi nchini kwetu. Mchango wake
katika kupigania Demokrasia nchini ni wa kupigiwa mfano na Kwa Kweli wengi wetu
Leo tunafaidi matunda ya Vyama vingi Kwa sababu ya kazi kubwa ambayo Mzee
Ndesamburo na wenzake walio hai na waliotangulia mbele ya haki walifanya. Mzee
Ndesamburo amechangia Sana ukuaji wa sekta ya utalii nchini. Kupitia kampuni
zake za Keys Hotels ameweza kuchangia Sana ukuaji wa sekta ya Utalii nchini
kwetu. Bungeni alikuwa mstari wa mbele kutaka uhifadhi wa mlima Kilimanjaro
kutokana na tishio la theluji kuondoka katika uhai wetu ( in our life time).
Kwa hakika Vyuo Vikuu vyetu vya Umma vingekuwa vinatenda haki Mzee Huyu
angepewa Shahada ya Uzamivu ya Heshima Kwa mchango wake katika Maendeleo ya
sekta ya Utalii nchini kwetu. Nawapa pole Sana watoto, wajukuu na vitukuu vya
Mzee Ndesamburo. Mzee wetu aliishi maisha yake na ameacha ‘ legacy ‘ yake.
Najua maumivu yenu lakini tupo wengi tunaoumia nanyi. Mungu awavushe kwenye
mtihani huu mkubwa. Muwe wamoja na mshikamane. Poleni Sana ndugu zangu wa CHADEMA
Kwa kupotelewa na Kiongozi wenu na Kiongozi wetu pia. Poleni Sana wana Moshi
Mjini na wana Kilimanjaro wote. Poleni Sana Watanzania. Pumzika Kwa Amani
Philemon Kiwelu Ndesamburo. Hiyo ni njia yetu sote. Amina”
|
Zitto Kabwe |
0 Comments:
Post a Comment