Monday, May 22, 2017

Vituko vya Machinjioni: Vingunguti

Wanunuzi wawili wa nyama ambao majina yao hayakufahamika mara moja katika machinjio ya Vingunguti jijini Dar es Salaam wakirushiana makonde katika eneo lenye kinyesi cha ng’ombe na mbuzi baada ya kutofautiana katika uchaguaji wa nyama huku mmojawapo akiwaamulia wasiendelee kupigana. 
Wengi wanafahamu kuwa siku njema huonekana asubuhi. Wataalamu wa Saikolojia wanaamini kuwa siku njema huanza siku ya nyuma yaani jana. Ikiwa na maana kuwa ili siku iwe njema maandalizi yake huanza jana na kesho yako ni kwasababu ya leo ulivyoiandaa. Iwe kwa jambo zuri au baya yote hayo ni kutokana na maandalizi yako siku ya nyuma. Kama inavyoonekana picha kituko hiki kilitokea katika machinjio ya mifugo ya Vingunguti jijini Dar es Salaam saa 3 asubuhi ya Mei 21, 2017  pale wanunuzi wawili ambao majina yao hayakufahamika mara moja waliposhindwa kuelewana na kupeana songombingo la hatari lililowatoa udenda hata kusukumiana kwenye uchafu wa machinjioni hapo.




0 Comments:

Post a Comment