Monday, May 22, 2017

Leo ni siku ya Wabaha'I

Alama ya Wabaha'I
Jumuiya ya Wa-Bahai waishio Dar es Salaam leo inaungana na jumuiya nyingine za madhehebu hayo kote ulimwenguni kwa ajili ya kusherehekea Tangazo la Bab.
Bahá'u'lláh_(Mírzá_Ḥusayn-`Alí_Núrí) mwaka 1868
Katika taarifa yake Mwakilishi wa Vyombo vya Habari wa Baraza la Kiroho la Wabaha’I wa Dar es Salaam Qudsiyeh Roy amesema tangazo la Bab ni mojawapo ya siku takatifu tisa kwa mujibu wa imani yao ambapo siku ya maadhimisho, Wabaha’I hawapaswi kwenda kazini ama Shuleni.

Roy amesisitiza kuwa kuwa imani yao inajitegemea, isiyopaswa kuunganishwa na imani nyingine kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakiilinganisha na dini nyingi kubwa hususani Uislamu.

Ibada fupi, usomaji wa maandiko matakatifu, burudani ya nyimbo, mazungumzo na chakula vitafanyika katika maadhimisho hayo.

Licha ya kusherehekea siku hii, wafuasi hao wa Bahaullah watakuwa wakitimiza miaka 174 tangu kuzaliwa kwa Imani ya Baha’I, mnamo Mei 22, 1844 Bab alikamatwa, kupigwa na kufungwa hatimaye aliuawa Julai 9, 1850 hadharani katika uwanja wa Tabriz nchini Iran.

Wabaha’I wanaamini kuwa wadhihirishaji wote wa Mungu ni pamoja na Ibrahimu, Krishna, Musa, Zoroasta, Budhaa, Yesu, Muhammad, Bab na Bahaullah ambao ni waelimishaji watukufu.

0 Comments:

Post a Comment