Raila Odinga akifanya maombi Jerusalem hivi karibuni. |
Mgombea urais kwa tiketi ya
Muungano wa Upinzani nchini Kenya (NASA), Raila Odinga anatarajiwa kuongoza
maelfu ya watu katika mkutano mkubwa wa kwanza akiwa na viongozi wa muungano
huo kwenye ngome za chama cha Jubilee kinachoongozwa na Rais Uhuru Kenyatta.
Hayo yanajiri baada ya
kumaliza safari yake ya kuhiji mjini Yerusalemu ambako Odinga alifanya maombi
katika mji huo mtakatifu kabla ya kuanza Kampeni za kuwani kiti hicho Agosti 8
mwaka huu.
Odinga anatarajiwa kurudi nchini
humo na kufanya mkutano huo Jumapili ya Mei 14 mwaka huu huko Nakuru katika
viwanja vya Afraha. NASA inaamini kwa kufanya mkutano katika eneo hilo tayari
wameshapata kura milioni 10.
Mratibu wa mkutano huo Boni
Khalwale amesema jana kuwa viongozi watano Kalonzo Musyoka, Musalia Mudavadi,
Isaac Ruto, Moses Wetangula na Raila wakitarajiwa kuhudhuria katika ngome hiyo
imara ya Jubilee.
Akiwa nchini Israel, Raila alizuru
ukingo wa Magharibi.
0 Comments:
Post a Comment