WELLINGTON, NEW ZEALAND
Chama tawala cha
New Zealand kimesema hakitajibu chochote baada mwanamuziki mashuhuri wa Marekani
Eminem kukipandisha chama hicho kortini.
Eminem |
Msemaji wa chama
hicho Steven Joyce amesema kwa sasa wanasubiri uamuzi wa mahakama kuhusu shtaka
hilo.
Jana mwanasheria
wa Eminem Garry Williams aliiambia
mahakama Kuu mjini Wellington kuwa chama tawala cha New Zealand kilitumia wimbo
wake ambao kwenye tangazo la kampeni bila idhini ya msanii.
Rapa huyo amesema
wimbo uliotumiwa katika tangazo la chama cha National Party mwaka 2014 ulikuwa
makala ambayo haikuwa imeidhinishwa ya wimbo wake wa Lose Yourself.
Lakini mawakili wa
chama hicho wanasema wimbo uliotumiwa haukuwa wa Lose Yourself, bali ni wimbo
ufahamikao kama Eminem-esque ambao waliununua kupitia soko la jumla la muziki
mtandaoni.
Katika kesi hiyo
iliyoanza jana na kutarajiwa kuchukua takribani siku sita, nyimbo zote mbili
zilichezwa katika ukumbi wa mahakama.
Wakili wa Eight
Mile Style, kampuni inayomuwakilisha mwanamuziki huyo, amesema wimbo wa Lose
Yourself ulikuwa na kipekee na bila shaka ni fahari ya kazi za sanaa za Eminem.
Tangazo hilo la mwaka
2014 lilikuwa na picha za wapiga makasia na sauti nyuma yake ikiwahimiza watu
kudumisha "timu ambayo inafanya kazi" na kurejesha National Party
madarakani katika uchaguzi uliokuwa unakaribia.
Wimbo uliotumiwa,
Eminem-esque, unakaribiana sana na Lose Yourself, ambayo ulitumiwa katika
filamu ya Eminem ya 8 Mile ambayo ilitolewa 2002.
0 Comments:
Post a Comment