Mzoga wa tembo baada ya kuuliwa na majangili |
MAUAJI ya tembo katika Mbuga
ya Selous yamepungua kutoka mizoga 184 hadi 84.
Hayo yanajiri wakati ambapo
tembo wawili kuuawa na wananchi hivi karibuni huku mmoja aking’olewa meno yake
katika kijiji cha Wenje Tarafa ya Nalasi wilayani humo.
Akizungumza katika kikao cha
Ulinzi na Usalama cha Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Kaimu Mkurugenzi wa
Operesheni ya kuuzuia Ujangili dhidi ya wanyama Pori Robert Mande amesema takwimu hizo zinaonyesha kuwa ukubwa
wa tatizo hilo umepungua kutokana na jitihada za kupambana na majangili.
Mande amesema mizoga ya tembo
imepungua kutokana na wafanyabiashara wakubwa wa pembe za ndovu kukamatwa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi
na Usalama wilaya ya Tunduru Juma Homera amewataka watu wanaomiliki Silaha
Kiholela kuzisalimisha kwenye ofisi za vijiji na vituo vya Polisi
Homera amebainisha kuwa wananchi
wanaoishi karibu na mipaka ya nchi jirani ya Msumbiji wanapata silaha hizo kwa
kubadilishana na chakula.
Kutokana na tukio hilo watuhumiwa
8 wa ujangili wamekamatwa
Kwa upande wake Mratibu wa
Shirika la PAMS Foundation
linalojishughulisha na Mapambano dhidi ya Ujangili Maximillan Janes amesema shirika limetoa ndege mbili ambazo
zinatumika kulinda wanyama wasiingie katika makazi ya watu pia kufuatilia
mienendo ya watu wanaojihusisha na ujangili.
0 Comments:
Post a Comment