Monday, May 29, 2017

Kufuturisha kwapigwa marufuku Zanzibar

Futari ya Mfungo wa Ramadhani

Serikali  ya  Mapinduzi  ya  Zanzibar  imepiga  marufuku  kuftarisha  katika  kipindi  hiki  cha  mwezi  mtukufu  wa  Ramadhan  pamoja  na uuzwaji  wa  vyakula  kiholela   hususani  vilivyopikwa  ikiwamo  juisi  isipokuwa  wa  maeneo  yaliyoruhusiwa  kisheria.

Marufuku hiyo imekuja visiwani humo ili kukabiliana na maradhi ya kipindupindu baada ya kutokea kwa visa 23 vya wagonjwa wa maradhi hayo hali ilisababisha kufunguliwa kwa kambi maalum katika Hospitali ya Chumbuni kwa wagonjwa wenye vimelea hivyo.

Akitoa  taarifa  hiyo  kwa  waandishi  wa  habari  Kaimu  Waziri  wa  Afya  Riziki  Pembe  Juma  amesema  kuwa  ugonjwa  wa  kipindupindu hususani  Unguja  umerejea  hivyo kuna haja ya kuweka mazingira ya usafi ili kuepuka maradhi hayo ikiwamo kuacha kufuturisha na kuongeza kuwa maeneo yanayoongoza kwa visa vya kipindupindu ni Mtoni Kidatu na Chumbuni.


Aidha serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeweka mikakati ya kukabiliana na maradhi hayo ikiwamo kutoa elimu kwa wananchi juu ya maradhi hayo.

0 Comments:

Post a Comment