Halmashauri ya Wilaya ya Moshi katika bajeti yake ya 2023/2024 imetenga kiasi cha shingi milioni 16 kupitia mapato yake ya ndani kwa ajili ya kuchimba bwawa la samaki ambalo litatumika kama shamba darasa ili kukabiliana na uvuvi harama kwenye Bwawa la Nyumba ya Mungu.
Wednesday, March 29, 2023
Bwawa la Samaki kuchimbwa Wilaya ya Moshi 2023/24
Wagonjwa wa Marburg marufuku kufanya tendo la ndoa
Baada ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuthibitisha visa vya wagonjwa wa Marburg mkoani Kagera ambako watu watano kati ya wanane walifariki dunia kutokana na virusi vya homa ya Marburg, sasa wa imebainika kuwa wagonjwa wa homa hiyo wanapaswa kujizuia kufanya tendoo la ndoa kwa mwaka mmoja.
Akizungumza
na Jaizmela News Mkurugenzi mtendaji
wa Hospitali Maalum ya Magonjwa Ambukizi Kibong’oto Dk. Leonard Subi, alisema, “Popo
ambao wanapenda kuishi kwenye maeneo ya mapango na wanyama wengine kama swala,
nyani na nguruwe wanaweza kuwaathiri binadamu kutokana na kuwa karibu na mnyama
lakini pia kula nyama yake.”
Aidha
Dk. Subi aliongeza, “ Unapoingia kwa binadamu virusi hivyo vinaweza
kumwambukiza mtu mmoja hadi mwingvine kwa kugusana, kushikana mikono, majasho,
mikono au kujami.”
Katika
suala la kujamiana (kufanya tendo la ndoa) Dk. Subi alisema, “ sisi hatuzuii
kujamiana kama watalaamu tunakushaurui njia nzuri ya kujamiana ili
usimwambukize mwenza wako, kwanza kwa kufanya ufuatiliaji, mtu mwingine anaweza
kuathirika kwa virusi vya Marburg bahati nzuri akapona sife, lakini bahati
mbaya pia akaendelea kufanya tendo la ndoa baada ya siku 21 huwa tunamfanyia
ufuatiliaji.
Dk.
Subi alisisitiza kuwa virusi vya Marburg vinaweza kukaa katika shahawa kwa
mwaka mzima hivyo hatari ya kuambukizwa ni kubwa wa waliothirika na wakapona.
Hata
hivyo Dk. Subi alisema Hospitali ya Kibong’oto imeshatuma wataalamu mkoani
Kagera kwa ajili ya utafiti huku wengine wakiwa tayari endapo maradhi hayoi
yatasambaa nchini.
Shirika
la Afya Duniani WHO lilisema, “Mwonekano wa wagonjwa katika awamu hii
umeelezewa kuwa unaonyesha sifa za kama mizimu, macho ya ndani, nyuso zisizo na hisia na uchovu mwingi.”
Mnamo
Machi 21, 2023 Waziri wa Afya Ummy Mwalimu alisema serikali imefanikiwa kuuzuia
ugonjwa huo kutoka nje ya mipaka ya ya mkoa wa Kagera.
Ugonjwa
huo huambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine au kutoka kwa mnyama
kwenda kwa binadamu na unatajwa kutokuwa na tiba bali hutibiwa kwa dalili
husika anazokuwa nazo mtu.
Popo
wa Matunda aina ya Rousette wa nchini Misri mara nyingi huwa na virusi. Nyani
wa kijani kibichi na nguruwe wanaweza kubeba.
Miongoni
mwa binadamu huenea kupitia maji ya mwili na malazi yaliyochaful;iwa nao na
hata wakipona, damu au shahawa zao, kwa mfano zinaweza kuwaambukiza wengine kwa
miezi mingine baadaye.
DALILI ZA MARBURG
Unaanza
ghafla na Homa, Kuumwa vibaya kichwa, kuumwa misuli na baada ya siku tatu
hufuatwa na kuharisha , kuumwa na tumbo, kichefuchefu na kutapika.
Mkurugenzi mtendaji wa Hospitali Maalum ya Magonjwa Ambukizi Kibong’oto Dk. Leonard Subi, akizungumza na waandishi wa Habari mnamo Machi 28, 2023 mjini Moshi. |
Monday, March 27, 2023
Rais wa WABA ataka bima kwa mabondia
Akizungumza
na Jaizmela News Onesmo Alfred Ngowi alisema tasnia ya ndondi imekuwa
ikikabiliwa na changamoto lukuki kutokana na ukosefu wa sheria za kuendesha
ngumi za kulipwa.
“Kuna
tatizo kubwa sana ambalo linapaswa kutatuliwa kwa haraka zaidi, kwa mfano
nchini Tanzania Mfumo wake wa ngumi
hususani wa michezo yote ya kulipwa ni lazima iweze kutungiwa sheria, kwani kwa
sasa hivi hakuna sheria ya kuendesha ngumi za kulipwa au michezo ya kulipwa
hapa nchini, bali kuna Sera ambayo ilitungwa bila kushirikisha wà dau wote wa
michezo ya kulipwa,” amesema Ngowi.
Rais wa World Alliance Boxing Association (WABA) Onesmo Ngowi |
Ngowi
alisema kinachofanyika kwa sasa nchini ni sera tu inayotumika katika kuendesha
ngumi za kulipwa.
“Tunaiomba
Serikali kupitia Wizara inayohusika na michezo pamoja na taasisi zinazohusika
na michezo kupeleka hoja bungeni ya kutungwa kwa sheria itayosimamia michezo ya
kulipwa hapa nchini. Sheria hiyo itakapoundwa itakuwa na uwezo wa kusimamia
kwa.usahihi tasnia ya ngumi za kulipwa kuanzia Uaandaji, kumlinda bondia
mwenyewe, ili aweze kupata haki zake,” ameongeza Ngowi.
Ngowi
alisema mapromota walio wengi wamekuwa wakiandaa mapambano ya ndondi na
kuwalipa ujira kidogo mabaondia kutokana
na uksoefu wa sheria na mikataba thabiti.
“Lazima
kuwe na sheria inayosema mkuzaji (Promoter) anatakiwa.kuwa na sifa zipi ,
afanyeje ili aweze kuanza kupromoti ngumi, hapa nchini, analindwaje katika
sheria hiyo, bondia anapoumia akiwa mchezoni anatakiwa kupata msaada gani,
akishastaafu ngumi atakuwa akipata msaada gani,
bondia analindwaje katika mikataba hiyo , viwango vya kutoa fedha
kwa bondia, kucheza katika mapambano zinatakiwa
kuanzia viwango gani,” amesema.
Aidha
Ngowi aliweka bayana suala la mabondia weusi wanaopambana katika nje ya bara la
Afrika kuwa wamekuwa wakinyimwa fursa
nyingi za kushiriki mashindano ya ngumi huku akisisitiza kuwa bado ubaguzi wa
rangi michezoni hususani katika ngumi haujatokomea kwa kiwango cha kuridhisha.
Hata
hivyo Ngowi alisema uwepo wa WABA umesaidia pakubwa kwa mabondia wa Kiafrika kupata
fursa za kushiriki mashindano ya ngumi ikilinganishwa na hapo kabla ya
uanzishwaji wa Shirikisho hilo la Vyama vya Ngumi Duniani.
“Mabondia
wengi duniani hususan weusi wamekuwa wakitumika kama chombo cha kutengeneza
ulaji kwa mabondia wa kizungu, weusi wamekuwa wakiishi maisha ya dhiki sana,
mpaka sasa nchi 99 zimmeshiriki katika mapambano ya ngumi tangu kuanzishwa kwa
WABA mnamo mwaka 2005.
Ngowi
alisisitiza kuwa WABA imekuja na mkakati wa kuwatengenezea bima za maisha,
kuumwa, mafao yaoa pindi wanapostaafu waweze kulipwa, lakini pia mabondia
watakao kuwa wakishiriki kwenye kwenye mapambano makubwa waweze kupata stahiki
zao ili kuweza kuendesha maisha yao na ya familia zao.
Thursday, March 23, 2023
"Twenzetu Serengeti Kilimanjaro Watumishi wa Royal Tour" yazipeleka taasisi 10 za umma kutalii Serengeti
Fahari ya Simba katika Hifadhi ya Serengeti |
Taasisi 10 za umma mkoani Kilimanjaro zimepelekwa kutalii mbuga yenye maajabu makubwa duniani ya Serengeti ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan katika kuhamasisha watanzania kufanya utalii wa ndani.
Hatua hiyo inaelezwa na wadau wa utalii nchini kuwa ni hamasa waliyoipata kutoka kwa Rais wa Awamu ya sita Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha miaka miwili tangu alipopokea kijiti kutoka kwa mtangulizi wake Hayati Dk. John Pombe Magufuli.
Machi 23,2023 Serikali ya mkoa wa Kilimanjaro ilitoa baraka zote zote kwa watumishi hao kwenda Serengeti, kuitambulisha dunia juu ya mazuri yaliyofanywa na rais Samia tangu alipoingia madarakani Machi 19 mwaka 2021.
Mbuga ya Serengeti yenye ukubwa wa kilomita za mraba 30,000 ipo katika maajabu saba ya Afrika na ipo katika orodha ya maajabu kumi ya vivutio vya asili duniani.
Zaidi ya watumishi 40 kutoka taasisi mbalimbali za umma mkoani Kilimanjaro, wameanza ziara yao ya kwenda kutembelea hifadhi ya taiafa Serengeti ambayo inatajwa kushika nafasi ya kwanza kwenye ukusanyaji wa mapato ikifuatiwa na hifadhi ya mlima Kilimanjaro.
Akiwaaga Watumishi hao Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro Dk. Vedasto Makota, amesema Samia amefanya juhudi kubwa katika kuutangaza utalii ndani na nje ya nchi, kitendo walichokifanya watumishi hao ni jitihada za kumuunga mkono rais Samia katika kuhamasisha utalii.
"Ninyi kama watumishi wa umma mmejenga taswira njema kwa serikali yenu ya kuhamasisha utalii wa ndani, hivyo mtakaporudi tunatarajia mtakuwa mabolozi wazuri wa kuutanza utalii wetu,"amesema Dk. Makota.
Amefafanua kuwa "Hifadhi ya Taifa ya Serengeti imejizolea umaarufu mkubwa duniani baada ya Simba mkongwe maarufu "Bob Junior" aliyeuawa na wanae ili kumaliza utawala wake duniani baada ya kuwa mfalme wa nyika akiongoza zaidi ya Simba 3000 walioko katika hifadhi hiyo,"amesema.
Kwa upande wake Mratibu wa "Twenzetu Serengeti Kilimanjaro Watumishi wa Royal Tour" Rashid Ally Rashi amesema kuwa katika kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Rais Samia yako mafanikio makubwa aliyoyafanya ikiwemo kuondoa kodi kwenye bodi ya mikopo, pamoja na kupandisha madaraja kwa walimu.
Akizungumza Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini TARURA Mkoa wa Kilimanjaro Mhandisi Nicholas Francis, amesema kuwa Serikali imeweza kuwaongezea bajeti kwa asilimia 185 ambapo TARURA ilikuwa ikipata shilingi bilioni 9.2 lakini katika bajeti ya 2022/2023 wameongezewa shilingi bilioni 33.19.
Nao baadhi ya Watumishi wanaoshiriki ziara hiyo Exzaud Mtei, Julia's Kibwana na Basila Mmbaga, wamesema kwenye sekta ya elimu wameshuhudia uboreshaji wa miundombinu ya shule, ikiwemo ujenzi wa shule mpya nyingi nchini kote; hali ambayo imewezesha wanafunzi wengi kupata nafasi ya kupata elimu kuanzia ile ya awali hadi elimu ya juu.
Aidha wamesema eneo lingine ni kwenye sekta ya utalii, kilimo na afya ambapo wamesema kuongezwa kwa bajeti kwenye sekta hizo chini ya uongozi wa Rais Samia kumewezesha huduma za kijamii kuboreshwa nchini.
TANESCO, TARURA, MUWSA, POLISI, ARDHI, MALIASILI, ELIMU, AFYA ni miongoni mwa taasisi za umma zinashiriki ziara hiyo katika Mbuga ya Serengeti kwa udhamini wa Zara Tours.
RC BABU: Wataalamu wa Afya simamieni kikamilifu ukusanyaji mapato vituo vya afya
Wednesday, March 22, 2023
Mahafali ya Kidato cha Sita Wasabato-Hai 2023 yalivyofana, Dk. Subi mgeni rasmi
Vijana wa Kanisa la Waadventista (Wasabato), wametakiwa kuwa wazalendo na waaminifu kwa nchi yao ili kuwa kielelezo kwa jamii inayowazunguka.
KUELEKEA SIKU YA KIFUA KIKUU MACHI 26: Hospitali ya Kibong’oto kufanya usafi makaburi ya wahanga wa kifua kikuu, kutoa elimu Mererani
Hospitali Maalum ya Afya ya Jamii na Magonjwa Ambukizi ya
Kibong’oto, inatarajiwa kufanya usafi katika makaburi ya wahanga wa kifua kikuu
waliofariki na kuzikwa hospitalini hapo enzi za ugunduzi na majaribio ya dawa waliokuwa
wakiletwa hospitalini hapo.
Akizungumza hivi karibuni na wajumbe wa Serikali wa
Kijiji cha Mae, viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kata ya Ibaeny pamoja na
viongozi wa dini waliotembelea hospitalini hapo kuelekea maadhimisho ya
kimataifa ya kifua kikuu Daktari bingwa na mtafiti wa magonjwa ambukizi Peter
Mbelele alisema kwa takribani miaka 60 tangu kugunduliwa kwa kimelea cha
ugonjwa huo kumekuwa na jitihada mbalimbali za kuhakikisha wanapunguza
uwezekano wa kusambaa zaidi kwa kifua kikuu.
“Wagonjwa wa kifua kikuu walikuwa wanatengwa na kuletwa
hapa kibong’oto takribani miaka 60 tangu kugunduliwa kimelea cha kifua kikuu
toka mwaka 1882 na mwaka 1943 ndipo kuligundulika kwa dawa ya kifua kikuu,”
alisema Dk. Mbelele.
Dk. Mbelele alisema tangu kuanza kwa Hopsitali ya Kibong’oto
mnamo mwaka 1926 wahanga wa ungonjwa huo walikuwa wakiletwa hapo na waliofariki
walizikwa katika eneo lililotengwa hospitalini hapo ambayo sasa imekuwa sehemu
ya historia.
“Mwaka 1926 ilipoanza kibong’oto ilianza kwa majaribio ya
kifua kikuu katika kuadhimisha siku ya kifua kikuu Machi 26 kibongo’oto ina
sehemu ya kihistoria ambako wahanga wa ugonjwa wa kifua kikuu waliokuwa
wakiletwa hapa kabla ya kugundulika kwa dawa hizo na wakati wa majaribio ya
dawa wengine walikuwa wanafariki na waliokuwa wanafariki walikuwa wanazikwa
hapa Kibong’oto,” aliongeza.
Hata hivyo Dk. Mbelele alisisitiza kuwa mwaka huu 2023
katika kuadhimisha siku ya kifua kikuu Machi 26 watumishi wa hospitali hiyo
watafanya usafi katika makaburi hayo ya kihistoria.
“Hekari nane za makaburi ambapo miili ya watu wa ugonjwa
waliofariki kwa ugonjwa wa kifua kikuu wamelazwa. Tutafanya usafi hapo,”
alisema Dk. Mbelele.
Pia aliongeza kuwa watakwenda mkoani Manyara katika
machimbo ya Tanzanite eneo la Mererani kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu Kifua
Kikuu.
Hospitali ya Kibongo’oto inaongoza kwa nchi za kiafrika
kwa kupunguza muda wa matibabu
Mwaka 2017 hadi Juni 2022 iliweza kuwafikia wachimbaji
8000 na kati yao 850 waligundulika kuwa na kifua kikuu na kuweza kuwaweka
kwenye matibabu.
Watu 716 kati yao waligundulika kuwa na ugonjwa wa siko seli. Watu 15000 wamefikiwa kwa kutumia gari tembezi la Hospitali ya Kibong’oto.
Tuesday, March 21, 2023
Hospitali ya Kibong’oto yawatoa hofu wananchi kusambaa kwa vimelea kutoka maabara ya kisasa
Mitambo maalum katika maabara mpya ya kisasa katika Hospitali Maalum ya Afya ya Jamii na Magonjwa Ambukizi ya Kibong’oto, Siha mkoani Kilimanjaro
Hospitali
Maalum ya Afya ya Jamii na Magonjwa Ambukizi ya Kibong’oto, Siha mkoani
Kilimanjaro imewatoa hofu wananchi wanaozunguka maabara mpya ya kisasa
iliyojengwa kwa ajili ya uchunguzi wa vimelea vya magonjwa ambukizi baada ya
sintofahamu kuibuka ya uwezekano wa kusambaa kwa vimelea hivyo kwenye makazi ya
watu.
Akizungumza hivi
karibuni na wajumbe wa Serikali wa Kijiji cha Mae, viongozi wa Chama cha
Mapinduzi (CCM) kata ya Ibaeny pamoja na viongozi wa dini waliotembelea maabara hiyo Dk. Bingwa na mtafiti wa magonjwa ambukizi
Peter Mbelele aliwahakikishia viongozi hao kwamba mitambo iliyowekezwa kwenye
maabara hiyo hairuhusu vimelea kutoka nje ya jengo hilo na kwenda
kwenye makazi ya watu kwenda kuwaambukiza.
Dk. Mbelele
alisema serikali imewekeza kiasi cha shilingi bilioni 12.5 kwa ajili ya kujenga
maabara hiyo lakini pia imetoa fedha kiasi cha shilingi bilioni 10 kwa ajili ya
kununua mitambo iliyofungwa kwenye jengo hilo.
"Kukamilika
kwa Maabara ya Afya ya Jamii ngazi ya 3 ya usalama iliyoko kwenye hospitali
maalumu ya magonjwa Ambukizi-Kibong'oto Itachangia katika udhibiti wa kusambaa
kwa mgonjwa duniani na hivyo kuimarisha uchumi na usalama wa
binadamu,"alisema Dk. Mbelele
Aidha, Dk.
Mbelele alisema maabara hiyo itafanya ufutiliaji wa usugu wa vimelea kwa dawa
zinazotumika kwenye matibabu ya magonjwa mbalimbali na kufanya tathimini ya
kiwango cha dawa mwilini.
Kwa upande wa utafiti Katibu Mkuu huyo alibainisha kuwa maabara hiyo itafanya pia tafiti mbalimbali na ubunifu (innovation) katika sayansi ya tiba na kinga katika ugunduzi wa Dawa, Vitendanishi, Vifaa tiba pamoja na kutengeneza chanjo mbalimbali za kuzuia na kukinga magonjwa ambukizi.
Pia aliongeza
Hospitali ya Kibong’oto itatunza vimelea vya magonjwa mbalimbali ikiwemo
vinasaba vya vimelea mbalimbali Kutoa mafunzo ya kiuchunguzi na ubunifu kwa
wataalamu mbalimbali katika sekta ya Afya.
Hata hivyo
alisema maabara hiyo inatarajia kuboresha huduma za tiba, kupunguza gharama
ambazo Serikali inaingia katika kupeleka sampuli nje ya nchi kwa uchunguzi.
Kwa upande
wake Meneja wa Maabara ya Afya ya Jamii Kibong’oto Dk. Shaban Mziray, aliwatoa
hofu viongozi hao kwamba mitambo na vifaa vilivyowekwa katika jengo hilo iko
kwenye uangalizi wa halai ya juu.
“Usalama wa miundo mbinu ya maabara imeimarishwa ili kuthibiti upotevu vimelea, ambapo kuna mitambo ya Sisteam camera pamoja na walinzi kutoka kampuni binafsi,” alisema Dk. Mziray.
Dk. Mziray alisema
uwepo wa teknolojia za kisasa zaidi
kwenye.kifua kikuu imesaidia kubainisha aina ya kifua kikuu, kimelea cha kifua
kikuu, pamoja na usugu wake wa dawa.
Diwani wa
Kata ya Ivaeny Elinisaa Kileo aliushukuru uongozi wa hospitali hiyo kwa kuweza kuwapokea na kuweza kujionea
uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali katika kata yake, amemshukuru mtafuti
kwa kuwatoa hofu wananchi kwamba hakuna
madhara yeyote ambayo yanaweza kutokea kwa wananchi walio karibu na maabara
hiyo kuambukizwa na vimelea.
Katibu wa
CCM Kata ya Ivaeny Reuben Munuo na mwenyekiti wa kitongoji Grace Mmari,
wamemshukuru Rais samia kwa kufanikisha ujenzi wa maabara hiyo kwani itakwenda
kusaidia watanzania wengi.
Aidha
Mchungaji Osca Tarimo na Lameck Kileo, walimshukuru Diwani wa kata hiyo kwa
kuwaandalia ziara ya mafunzo kwa ajili ya uwekezaji uliofanywa na serikali
ndani ya wilaya ya siha.
Hospitali ya
Kibong’oto ina jukumu la kutoa huduma za Afya ya jamii na ufuatiliaji wa
magonjwa yote yenye umuhimu katika jamii yaliyoaninishwa na Shirika la afya
Duniani (WHO) na yale ya mlipuko.
Thursday, March 16, 2023
NFRA yatoa tani 256 za chakula wilayani Mwanga
Serikali kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya chakula (NFRA) imetoa tani 256 za chakula kwa wananchi wa wilaya ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro, hatua ambayo itasaidia kukabiliana na upungufu wa chakula wilayani humo.
Akutwa na vipande 6 vya meno ya Tembo
Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia mwanaume mmoja mkazi wa Wilaya ya Same, kwa tuhuma ya kupatikana na vipande sita ya meno ya tembo.
Saturday, March 11, 2023
Miaka 2 ya Rais Samia: Jumuiya ya Wazazi CCM-Hai yampongeza
Baraza la Jumuiya ya Wazazi (WAZAZI) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, kimempongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na serikali yake ya awamu ya sita kwa kazi nzuri ambayo imeboresha maisha ya Watanzania wengi ndani ya miaka miwili ya utawala wake.