NA MWANDISHI WETU
TANESCO |
Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO), limesema maeneo yote
yaliyounganishwa kwenye mfumo wa taifa wa kusambaza umeme asubuhi ya leo
yaliathirika na kukatika kwa ghafla kwa umeme kutokana na hitilafu katika
mtambo wa kupooza na kusambaza umeme eneo la Ubungo jijini hapa Dar es Salaam.
Umeme ulikatika ghafla saa kumi na mbili na dakika 32 asubuhi hali
ambayo iliibua sintofahamu kutokana na shughuli nyingi kuendeshwa kwa nishati
hiyo.
Kituo hicho cha Ubungo ni kituo kinachotumiwa kudhibiti na kusambaza
umeme mikoa yote ukiondoa mikoa ya Kagera na Kigoma inayopata umeme kutoka nchi
jirani ya Uganda.
Kaimu Meneja uhusiano wa Tanesco, Leila Muhaji amesema wataalam
wanaendelea kushughulikia tatizo hilo ambapo mtambo wa kilovolti 220 ulipata
hitilafu
Aidha hitilafu hiyo imeathiri mitambo ya kusukuma maji katika ya
DAWASCO, mitambo mitatu ya Ruvu Juu, Ruvu Chini na mtambo wa mtoni hivyo huduma
ya maji kukosekana kwani mitambo hiyo hutegemea umeme kufanya kazi.
Kwa upande wake Kaimu Meneja uhusiano wa Shirika la Maji Safi na Maji
Taka jijini Dar es Salaam Evalastin Liyaro amesema baadhi ya maeneo
yanatarajiwa kukumbwa na uhaba wa maji ama kukosa huduma hiyo kwa muda
usiojulikana.
CHANZO: BBC
0 Comments:
Post a Comment