NA MWANDISHI WETU
Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dar es Salaam |
WATANZANIA
wametakiwa kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ili waweze kupata
matibabu kwa unafuu kutokana na gharama kuwa juu hususani magonjwa ya moyo.
Akizungumza
wakati wa kuiaga timu ya wataalamu kutoka Hospitali ya Apollo, Bangalore ya
nchini India iliyotua katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya upasuaji wa moyo kwa wagonjwa
sita Dk. Bashiri Nyangasa alisema wananchi wa kawaida hawawezi kuzimudu gharama
za matitabu hayo.
Dk.
Nyangasa alisema watalaamu hao wameisaidia serikali kuokoa kiasi cha zaidi ya
shilingi Milioni 174 kwa wagonjwa hao endapo wangesafirishwa kwenda nje ya nchi
kwa matibabu.
Aidha
alisema upasuaji huo wa kuvuna mishipa ya damu mguuni na kuipandikiza katika
mishipa ya moyo iliyokuwa imeziba kwa wanaume wanne na wanawake wawili
umefanyika bila kutumia mashine ya mapafu na moyo.
JKCI |
Kwa
upande wake Dk. Sathyaki Nambala aliyeiongoza timu hiyo kuanzia Januari 12 hadi
Januari 16 mwaka huu amesema watoto wenye umri kati ya 10 na 18 ni waathirika
wakubwa wa magonjwa ya moyo na kuongeza taaasisi hiyo imejitahidi kuongeza
vifaa na kwamba utalaamu waliouacha utaweza kuokoa kiasi kikubwa cha fedha siku
za usoni.
Dk. Bashir Nyangasa akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kwenye Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. |
Hata
hivyo ujio mwingine wa timu ya watalaamu kutoka kambi ya Madaktari Afrika
inatarajia kutua nchini Januari 23 na kufanya upasuaji wa bila kufungua kifua
kwa wagonjwa 15 huku Februari 4 ujio wa madaktari bingwa kutoka Saudia Arabia
utawasili na kufanya upasuaji wa aina hiyo kwa wagonjwa 55 wenye miaka 12 na
kuendelea.
0 Comments:
Post a Comment