NA MWANDISHI WETU
NA MWANDISHI WETU
Mfanya biashara maarufu wa madini
jijini Arusha, Venance Moshi (30),
amepandishwa kortini katika kesi inayomkabili ya kushambulia na kumjeruhi mkewe kwa chupa usoni ,wakiwa wanasuluhishwa
na baba mkwe, mgogoro wa ndoa yao.
Mwendesha Mashtaka Agnes Hyera mbele ya Hakimu Mkazi Devota Msofe alidai
Machi 11 mwaka jana maeneo ya Moshono jijini hapo mshtakiwa alinyanyua bilauri
na kumpiga kwenye jicho la kulia mlalamikaji Agnes Joseph.
Aidha mwendesha mashitaka alidai kitendo hicho kilimsababishia
mlalamikaji atokwe na damu nyingi.
Mshtakiwa alikana mashtaka hayo ambapo Hakimu Hyera ameiahirisha hadi
Februari 6 mwaka huu itakapotajwa tena.
0 Comments:
Post a Comment