NA
MWANDISHI WETU
BARAZA
la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne
na maarifa uliofanyika Novemba mwaka jana huku Dar es Salaam ikionekana kufanya vibaya
kuliko mikoa mingine nchini.
Aidha
imebainika katika matokeo hayo ufaulu katika masomo ya Historia, Kiswahili,
Hisabati, Fikizia, Book Keeping na Commerce umeendelea kushuka ukiwa chini ya
asilimia 50.
Akitangaza
matokeo hayo leo Katibu Mtendaji wa NECTA Dkt. Charles Msonde amesema watahiniwa
277,283 sawa na asilimia 70.09 wamefaulu kati ya watahiniwa 408,372.
Dkt.
Msonde amesema kiwango cha ufaulu kimeongeza kwa asilimia 2.56 ukilinganisha na
mwaka 2015 ambao ufaulu ulikuwa asilimia 67.06
Pia
shule ya Feza Boys ya Dar es Salaam imeongoza kwa ufaulu ikifuatiwa na St. Francis
Girls ya Mbeya na nafasi ya tatu ikishikwa na Kaizirege Junior ya Kagera.
Dkt.
Msonde ameongeza kuwa shule sita kati ya kumi zilizofanya vibaya katika mtihani
huo zinatoka Dar es Salaam ambazo ni Kitonga, Nyeburu, Mbopo, Mbondole,
Somangira Day na Kidete.
Mkoa
wa Dar es Salaam
haumo katika nafasi kumi za juu huku Njombe ikishika nafasi ya kwanza kwa
ufaulu ikifuatiwa na Iringa na nafasi ya tatu ikishikwa na Kagera.
Wakati
huo huo NECTA imefuta matokeo ya watahiniwa 126 kutokana na sababu mbalimbali
ikiwamo udanganyifu.
Dkt
Msonde amesema wanafunzi 60 walikutwa na vibuti huku watahiniwa 52 wakionekana
kufanana majibu.
0 Comments:
Post a Comment