NA
MWANDISHI WETU
MWANAFUNZI
wa sekondari ya Feza Boys ya jijini Dar es Salaam Alfred Shauri ameongoza
katika ufaulu wa mtihani wa kidato cha nne uliofanyika Novemba mwaka jana.
Gazeti la Tanzania Daima Februari 1, 2016 |
Aidha
Cynthia Mchechu wa shule ya sekondari ya St. Francis ya Mbeya ameongoza kwa
ufaulu kwa wasichana nchini.
Katibu
Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania
(NECTA), Dkt. Charles Msonde amesema wanafunzi hao wanastahili pongezi kwa
kufanya vizuri.
Wanafunzi
wengine waliofanya vizuri ni Erick Mamuya wa Marian Boys ya Pwani, Jigna Chavda
wa St. Mary Goreti ya Kilimanjaro, Naomi Tundui wa Marian Girls ya Pwani,
Victoria Chang’a wa St.
Francis na Brian Johnson wa Marian Boys.
Aidha
Esther Mndeme wa St.
Mary’s Mazinde Juu mkoani Tanga, Ally Koti wa ALCP Kilasara mkoani Kilimanjaro
na Emmanuel Kajege wa Marian Boys wameingia katika kumi bora.
0 Comments:
Post a Comment